Kuna vyeo vya kikatiba na visivyo vya kikatibam vyeo vya Kikatiba kwa mujibu wa Katiba ya JMT ya 1977 ni kama Urais wa JMT, Makamu wa Rais, PM, Mawaziri, AG, DAG,DPP, CAG, Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu etc. Vyeo visivyo vya kikatiba mojawapo ni kama uIGP, uCDF etc. Vyeo hivi visivyo vya Kikatiba msingi wake hutokana na sheria inayounda vyombo husika ambayo hutamka aina ya vyeo katika chombo husika. Aidha, vyeo visivyo vya kikatiba mara nyingine msingi wake huwa muundo wa vyombo husika ambao huandaliwa kwa kushirikisha chombo husika na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kwa mantiki hiyo basi cheo cha Naibu IGP hakipo katika Katiba lakini kimo katika Muundo mpya wa Utumishi wa Jeshi la Polisi. Hivyo, hakuna uvunjaji wowote wa Katiba uliofanyika.
Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums