Yes, it's a class struggle: Ni kwamba Daily nation ni mali ya Aga Khan Foundation, kama zilivyo AiR Uganda na Serena chain of hotels. Unilever, ilianzia huko Dublin miaka ya 1926 na leo ni a true multinational ikiwepo mabara yote isipokuwa antarctica, kwa maana ndiyo supplier wakubwa wa consumer products kwenye soko hili. EABL ni mali ya Diageo. KQ wakenya wana nadhani 25% stake, na KCB ni mali ya wahindi. Kwa upande mmoja Nakumatt na Uchumi mtaji wake uliporwa kwenye hela za wananchi maskini waKenya ambao pia walishanyan'gagwa ardhi yao. Hivyo hivyo brookside ya Uhuru Kenyatta mtaji wake ndio ungejenga vyuo vikuu vya umma na mahospitali ya wakenya maskini. Hapa kwetu, Bank M ya fisadi Mkapa, na mali kibao za vibaraka wake zingefanya vitu vikubwa kwa ajili ya mtanzania maskini ambaye ameporwa mali zake na viongozi wahaini, wasaliti na wauaji. Ndio maana wanaweza kutembelea magari ya milion 800 na hakuna anayweza kusema. Hawa watu walikuwa wa kuwa cremated au kufungwa maisha na kunyag'anywa kila kitu, lakini nani atafanya hivyo? State machinery wameinunua, ni miungu watu, wanafiki. Wangeweza kula na kushiba na wakafanya vizuri, lakini wakaamua kuteketeza kila kitu na kuharibia wananchi, kazi tunayo! Maana hakuna wa kuwauliza! Wote tuko kwenye shit moja, isipokuwa sisi haya ni mapya kwetu, sasa tuwe makini angalau huu unyama usilete maafa. Ninachosema, nadhani wakenya wao walishazoea maana hawajitambui, sisi pia yametokea ila tukizidi kuyaruhusu damage itakuwa beyond repair, if we shout we can salvage something esp land and employment. Kwa hiyo mwananchi maskini, iwe Mkenya au mtanzania hana lake, ingawa simaanishi kuwa tuwakaribishe wageni bila kuangalia interest zetu kwanza, if anything Wakenya wawadai viongozi wao waliowapora..maybe we can borrow a leaf, but we should be doing the same as well.
Ona Moi anamiliki dola bilioni tatu, kiongozi wa umma, huyu ni mwizi kama alivyo Mkapa na genge lake, kwa hiyo Mkenya anaposema wako ahead, ni kutojitambua, if we r not careful tutanyang'anywa kila kitu na sisi. CCM mpaka ipasuke yenyewe, kuiondoa kama yenyewe kazi ni ngumu, bado wanatumia mgongo wa Nyerere, na vijijini watu hawajui kuwa CCM ya Mwalimu siyo ya sasa, after all, hawawezi ku-analyze. Ndiyo maana CCM wanapeta kwa kwenda mbele. Suluhisho, we need to create awareness kwa mabadiliko haya ili watanzania wayajue, tusichoke.[/QUOTE]
Mkuu Kanyabwoya, heshima mbele, you have raised a very interesting observation. I take it as a warning example. Viongozi wa Kenya, kama akina uhuru, moi, kamotho na wengine, wamewatafuna wananchi (kama akina smatta, nomasana, kayundi2 na wengine) na kuwafanya masikini wa kutupwa, hivi kwamba hawajui waende wapi. wamechanganyikiwa mpaka vikundi kama mongiki ndiyo vinaonekana ndiyo nafuu na mkombozi wa wakenya masikini.
tunataka ile hali isiwe imported kwetu plus other trashes, sasa please, naomba initiate onother thread ili tujadili jinsi ya kupambana na expected trashes such as crime, corruption, money laundering, children abuse in tourism (like the case of mombasa) drugs trafficing etc to get into our territory ''under the umbrella'' of eac. kwa sababu kufungua mipaka ya nchi ni sawa na kufungua madirisha ya nyumba ili upate hewa safi, haimaanishi hewa safi tu ndiyo itakayo ingia ndani ila hata inzi, mbu, vumbi, vyaweza ingia, vivyo hivyo katika shirikisho si mitaji, wafanyakazi na wafanya biashara wazuri tu ndiyo watakao ingia kama smatta anavyoamini kwa upeo wake mdogo wa kufikiri. tutegemee na tujiandae kuona vitu ambavyo hatukuwahi hata kufikiria ambavyo ni vibaya.
MUHIMU: tafadhali hiyo thread ipeleke kwenye mambo ya ndani (siasa za ndani). Pia mods Abt-tchaz tafadhali, usimruhusu smatta na wenzake tresspassing our discussion, i know for them pondering on the socio-economic matter is a vocabulary, they will distort our up building and couraging discussion.
Adhuhuri njema.