Soma kwanza sheria ndio utoe hoja.
Madaraka ya kutangaza hali ya hatari
Ibara ya 32 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
32.-(1) Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, Rais aweza kutangaza hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano au katika sehemu yake yoyote.
(2) Rais aweza tu kutangaza kuwa kuna hali ya hatari iwapo-
(c) kuna hali halisi ya kuvurugika kwa amani ya jamii au kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama; au
(d) kuna hatari dhahiri na kubwa, kiasi kwamba amani ya jamii itavurugika na usalama wa raia kutoweka katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote ambayo haiwezi kuepukika isipokuwa kwa kutumia mamlaka ya pekee; au
(e) karibu kutatokea tukio la hatari au tukio la balaa au la baa ya kimazingira ambalo linatishia jamii au sehemu ya jamii katika Jamhuri ya Muungano; au
(f) kuna aina nyingineyo ya hatari ambayo kwa dhahiri ni tishio kwa nchi.
(3) Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania bara nzima au Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara moja nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais.
Sidhani kama tumefikia stage ya Rais kutangaza hali ya hatari. Kwa vile mmeambiwa kumonitor hali ya usalama kwa masaa 24 yajayo haimaanishi kwamba hakuna usalama wa jamii. Watu tunaogopa usalama wetu dhidi ya majambazi. Nothing else.