Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Tetesi: Kikwete kumrithi Ban Ki-Moon

Mwaka 2016 anatoka magogoni nchi ikiwa na déni kubwa kuliko wakati wowote (hatakama alijenga barabara na madaraja ni kwa mikopo)
utendaji katika ofisi za serikali ulijaa urasimu na wafanyakazi wenye kiburi kutokana na mfumo wa kazi kwa kufahamiana.
wizi,ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za serikali vilikithiri hâta mtoto mdogo angejua hii nchi tunaibiwa.
madawa ya kulevya yalitamalaki huku tukiambiwa majina yapo lakini hatua zilizochukuliwa zikiwa hafifu kabisa.
migogoro ya wakulima na wafugaji,migomo ya walimu na wafanyakazi viwandani,na uchaguzi wa zanzibar navyo viliishinda diplomasia ya serikali na ubabe kutumika.
Vitendo kandamizi vyawatu kung'olewa meno,kumwagiwa tindikali na simu hatari na kesihizo kuishilia hewani bili uchunguzi wa kina na matokeo yenye uwazi viliitia doa serikali.
Na mengine meeeengi....chamuhimu unapomchambua mtu tuletee pande zake zote sio unasifiasifia tuuuu as if hana mapungufu! Hapo ndo tutajua Kama anaweza kukabiliana na changamoto ama la
 
HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON
_________________________________________________
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia.

Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.

Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.

Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.

2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.

Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.

Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.

Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .

Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...

2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.

View attachment 325689 View attachment 325692 View attachment 325693 View attachment 325694 View attachment 325695 View attachment 325696 View attachment 325697 View attachment 325698
Ama kweli watanzania wanachekesha, Huyu Kikwete aliyeshindwa nchi anaweza akapewa UN?? Thubutu....si huyu Kikwete ninayemfahamu....HANA UMAARUFU WOWOTE ZAIDI YA KUJIPENDEKEZA. Hizo Awards zinaweza kutolewa hata na magazeti ya mzalendo au uhuru au hata mashirika madogo yasiyofahamika ya kiushkaji. Sishangai hata jina la huyo aliyeleta hii thread inafanania kule kule.
 
Asije akataka kumrithisha riz 1 pindi akistafu!! / na akiulizwa swali malaika kwanini dunia imejaa na ufisadi pamoja na umaskini kwa safar hii nahisi atakuna............. Wadau naomba mjaze wenyewe!!
 
Mh Kikwete ukipata nafasi hiyo ifikirie Tanzania kwanza. Kila la Heri Honourable JK
Kama maajabu hayo yatatokea JK ataisahau TZ kabisa. Kama kwa miaka 10 unaamini watanzania walineemeka zaidi basi labda kuna kitu atafanya ingawaje hakuna anachoweza kufanya bila kwanza kuelekezwa na watakaompa kazi hiyo.

Itoshe tu kusema kuwa hiyo kazi hatapewa bila kwanza kukubali kuiuza Afrika yote kwa mabeberu wa magharibi!
 
Donald Trump akikusikia utaozea jela. Ni marufuku kwa Wafrika kuwa Katibu Mkuu wa UN.
Wanapaswa kutawaliwa upya!!

Zenji imshinde, yy aweze ya Israel VS Palestine/Iran? South Sudan vs Sudan? Burundi Vs Civilians/ Opposition? Nigeria Vs Bokoharam, Syria Vs IS, Iraq Vs IS ? North Korea vs S. Korea?
Mwenzie ana budget ya Tshs Trillion 22.99 LAKINI mfukoni ana Tshs Trillion 4!! Kisa wamekata!!

Hata katibu mkuu USA, na UK wanahusika sn kuamua nani awe na nani asiwe!!
 
Ndugu zangu historia inaonyesha kwamba HAKUNA NABII ANAE KUBALIKA KWAO.
Mifano hai ni Yesu na Muhammad (SAW) Imekuwa vigumu kwa mayahudi kumkubali Yesu, ni hivyo hivyo kwa maqureish kumkubali Muhammad (SAW).
Lakini ulimwengu mzima wanawakubali viongozi hawa wa dini.

........Kudos Brother Jakaya go on with our full blessings.
 
LAKINI hii ni zamu ya EUROPE kwa maana africa tayari bw. KOFFI ANNAN ikafuata zamu ya asia ya Ki Moon sasa ni Ulaya baadae North America,
Na iwe hivyo, ameshaiaibisha nchi akiwa rais, asije akatuaibisha kidunia pia, atulie na uzee wake hukohuko msoga, hao si wanajua ni rahisi kumtumia kuwadanganya waafrika wenzie, tangu lini mzungu akupe nafasi wewe mtu mweusi umuongoze!
 
pengine angeweza kubahatika kupata kupitia nguvu ya mashosti na wanafiki wenza USA....lakini tatizo amelikoroga kule Z'bar!

watampiga chini tu kabla hata hajainuka!!
 
Ndugu zangu historia inaonyesha kwamba HAKUNA NABII ANAE KUBALIKA KWAO.
Mifano hai ni Yesu na Muhammad (SAW) Imekuwa vigumu kwa mayahudi kumkubali Yesu, ni hivyo hivyo kwa maqureish kumkubali Muhammad (SAW).
Lakini ulimwengu mzima wanawakubali viongozi hawa wa dini.

........Kudos Brother Jakaya go on with our full blessings.
Shida yetu wabongo tunataka au tunafikiri watu wa dunia nzima wanaongozwa na fikira mgando kama zetu!! Huyu bwana aliingia madarakani (2005) akikiri kabisa mwenyewe kuwa Zanzibar kuna mpasuko wa kisiasa na hilo lingekuwa mojawapo ya vipaumbele vyake. Amemaliza utawala wake (2010) na si kuiacha tu Zanzibar katika mpasuko mkali, bali pia yeye mwenyewe kuchochea kuni katika mpasuko huo!! Alikuwa na fursa ya kipekee ambayo pengine hatotokea rais mwingine katika miaka kama 20 hivi ijayo kuipata ambapo ingeweza kutoa ufumbuzi muafaka wa mpasuko wa ZnZ lakini hakababaika na hiyo fursa ikamponyoka - Katiba Mpya! Ilimponyoka si kwa sababu nyingine zaidi ya uhifadhina wa kiCCM - wao bado wameshiklia na kuishi katika siasa za karne ya 20 (wameng'ang'ania muundo wa muungano wa serikali 2 ambao inawezekana ni kweli ulifaa sana kwa karne hiyo) wakati katika karne ya 21 huo muundo hauna tija tena! Wameshikilia dhana ya 'mapinduzi' ya karne ya 20, wakati hiyo dhana haina tija tena zaidi ya kuitumika kama zana ya propoganda kwa kikundi cha wateule wachache kuendelea kuhodhi madaraka. Woga, Woga, Woga wa mabadiliko. Huyu ndio umkabidhi UN ya karne ya 21 - give me a break!
 
Mwambieni huko hatoshi, miaka yake 10 madarakani hapa Nyumbani kila kitu ni shaghala bagala ni kama tunaanza upya.
 
haaaaaaaaaaaaaaaaa wakimpa nafasi hiyo naiama tanzania naenda kuishi Mbinguni ntajinyonga na anajua Mungu atanipokea Mbinguni.
 
Kikwete kafanya mengi makubwa na mema Tanzania hii kuliko Rais yeyote wa kabla yake.

Wenye kufikiri japo kiduchu wanaliona hilo lakini mahasidi wao kila jema kwao ni baya.
 
HUYU NDIYE MRITHI WA BAN KI-MOON
_________________________________________________
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania kwa awamu ya nne (2005 – 2015) ni miongoni mwa wanadiplomasia wakubwa duniani wenye ushawishi na uwezo wa utatuzi wa matatizo mbalimbali duniani, sio tu kwa sababu viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanamkubali bali kwa uwezo wake katika masuala ya kidiplomasia.

Alizaliwa mwaka 1950 Oct katika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Msoga katika familia ya kisiasa na kilimo. Baba yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Pangani na babu yake naye ambaye alikuwa ni Chief wa Wakwere, Chief Kikwete.

Alipata elimu ya Msingi Msoga kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Kibaha akiwa pia ni mwenyekiti serikali ya wanafunzi na vijana wa TANU 1966 na Baadaye Tanga school. Ambapo alijiunga na chuo kikuu Dar es salaam, ambapo pia alikuwa mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi na kuhitimu Shahada ya uchumi 1975 alipojiunga na Jeshi.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida 1977 na baadae kuhamishiwa Zanzibar kwa kazi maalum baada ya muungano wa TANU na ASP mpaka kufikia mwaka 1980 aliporudishwa makao makuu ya chama (CCM).

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa mbunge na pia NaibuWaziri wa Nishati na Madini chini ya uongozi wa MH. Al Ahsan Mwinyi mpaka kufikia mwaka 1990 ambapo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa maji nishati na madini.

Mwaka 1994 aliteuliwa kuwa waziri wa uchumi akiwa na umri wa miaka 44 ambapo alikuwa ni waziri mwenye umri mdogo kuwahi kuteuliwa. Kufika mwaka 1995 alitueliwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya uongozi wa Rais Benjamin W. Mkapa na kuongoza wizara hiyo kwa miaka 10 mpaka kufikia mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika Nyanja za kimataifa Mh. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wanadiplomasia ambae amefanya mambo mengi katika bara la Afrika na Dunia, kama vile kutatua migogoro katika nchi za maziwa makuu, jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa kama Mwenyekiti wake (EAC) baadhi ya mambo ambayo dunia inampongeza ni pamoja na Mwaka 2005 akiwa kama Mwenyekiti mwenza wa mikutano wa Helsinki (Helisinki process on Globalization and Democracy) aliweza kuongoza mikutano huo kwa mafanikio makubwa.

2013 akiwa ndiye kiongozi pekee kutoka Afrika aliyeshiriki katika mkutano nchi za umoja wa Ulaya EU wa Alpbach Austria aliliwakilisha bara la Afrika vyema katika kutafuta fursa za maendeleo na ushirikiano kimataifa.

Dr. Jakaya Kikwete pia amekuwa Mjumbe tume ya Elimu Duniani ikiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown katika kutafuta namna ya kugharamia Elimu duniani (TICFGEO) kwa mwaka 2015.

Kwa mwaka huu 2016 Dr. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mjumbe wa kamati ya Amani nchini Libya katika kusaidia kurudisha amani nchini Libya
Pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mwenza kwa tume ya kusaidia afya ya Mama na motto duniani kwa mwaka huu 2016 ikiwa ni katika jitihada zake kuhakikisha Afya na mama na motto duniani kote zinalindwa.

Kwa mtazamo huo nina imani kubwa kwa kipindi ambacho Mh. Ban Ki-Moon ataachia ofisi, Mwanadiplomasia huyu ndiye atakayechukua viatu vyake .

Hizi ni baadhi ya tuzo za heshima alizowahi kupata toka nchi mbalimbali...

2007: Sullivan Honor
2007: The AAI African National Achievement Award (on behalf of Tanzania).
2009: US Doctors for Africa Award.
2011: Social Good Award from the United Nations Foundation
2011: South-South Award for Global Health, Technology and Development
2012: FANRPAN Policy Leadership Award from the Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network.
2013: Africa's Most Impactful Leader of the Year by the Africa Leadership Magazine
2013: ICCF Mengha Award by the International Conservation Caucus Foundation
2014: Icon of Democracy Award, from The Voice Magazine (Netherlands)
2015: Leadership Excellence Award by the Pan-African Youth Union.
2015: African Achievers Award by the Institute for Good Governance in Africa.
2015: African Statesman of the Year by the The African Sun Times.

View attachment 325689 View attachment 325692 View attachment 325693 View attachment 325694 View attachment 325695 View attachment 325696 View attachment 325697 View attachment 325698
Hiyo sahau it wont happen.....we hujui siasa za kimataifa zinavyofanyika unadhani nje hawajui ujinga uliokuwapo hapa!!! Kuna waziri mstaafu wa New Zealand (Ex-New Zealand Premier Helen Clark to run for UN top job - BBC News) pia ame declare atagombania nafasi hiyo na naamini wako pia wengine wengi wenye uwezo na uzoefu wa masuala ya kimataifa mbali mbali sana na JK. Hata sijui ulieleta uzi huu kama uko makini au unaleta polojo za furahisha genge. Anyway maybe let me not be too harsh, sio mbaya kudhani na kujitukuza. Mtoto hudhani kuwa babake ndio mtu muhimu kuliko wote duniani hata kama ni lofa, mpaka akue. Nafikiri sio mbaya kurejea ile fasihi ya Ndyanao Balisidya kuna character anaitwa Chonya nafikiri kijiji cha Chilonwa walikuwa wanadhani ndio mjanja na mwelevu kuliko wote duniani, lakini wengi tulijua sio kweli, he was just a local hero....
 
Kwa nilicho sikia ni mama anaitwa Helen Clark
Ambaye ndie mwenye chance kubwa ya kuchukua hii top job.
 
Back
Top Bottom