Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,362
Reaction score
2,373
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

====

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.

Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.

Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."

Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.

Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.

"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”

"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.

"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.

Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.

Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.

Chanzo: Mwananchi
 
JK amesahau matumizi ya teknolojia hayabadilishi mitaala, usome kwa kutumia tablet au mwenzio aende kayumba at the end of the day wote watafanya mtihani mmoja.

Labda yule wa tablet atamzidi mwenzie topic alizo-cover in case ikitokea issue kama ya Corona, ila pasipokuwepo na Corona tofauti yao itakuwa ndogo sana.

Kitakachomyima mtoto wa masikini ajira hata akiwa na ufaulu mzuri bado ni kujuana (nafasi kutolewa kwa upendeleo) lakini sio kwasababu ya teknolojia, na ajira bado zitakuwepo pale pale haziwezi kuondoka.
 
Ajira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
 
Ajira zitatoweka vipi means panakuwa hamna Serikali, aache uongo Serikali hela ipo ya kutosha na tunataka kuona raia mnajenga nchi msiwe na wasiwasi.
2050 dunia itakua ktk elimwengu mwengine Wa sayansi, elimu ya "sikuile akaenda, shambani kutembelea, akayaona matunda, mtini yamejaa" haitokuwa na matumizi tena miaka hiyo! Tubadilishe mitaala!
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Teknolojia pia inatengeneza kazi nyingi, cha muhimu ni kuhakikisha watoto watu wanapewa kipaumbele kwa masomo ya sayansi na teknolojia ili hizo ajira nyingi zibaki nchini, hakuna teknolojia inayo ondoa ajira bila kutengeneza ajira nyingine.
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Kuzungumzia teknolojia leo wakati upatikanaji wa umeme tu bado ni shida ni mapema mno, mabadiliko ya teknolojia yatakuja pale ambapo tutajitosheleza kwa vitu vingine kama umeme, na wataalamu wa kutosha kufundisha.

Teknolojia itakapokuwa ndio itakuja kuathiri ajira za watu kama viwandani na kwingineko, lakini hapa kwetu bado wakati huo haujafika na sidhani kama tutafika 2050.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

Ajira zitatoweka kwa watoto wa masikini mnahamasisha maskini wazaliane ovyo kwa kuwazubaisha kuwa kusoma bure na ardhi ipo, na mnahamasisha kuthamini kiswahili mashuleni, lakini nyie watoto wenu mnawasomesha shule zenye mikondo ya kingereza international school ili kesho wawe watakaokuja kuhodhi ajira.
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Kwa hiyo hatutahitaji wawekezaji kutoka nje?
 
Back
Top Bottom