Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Watanzanina bado tunachujuliwa kama watoto wadogo. Pia watu wana shindwa kutofautisha ajira na utumwa
 
Easily manupulated
 
Teknolojia pia inatengeneza kazi nyingi, cha muhimu ni kuhakikisha watoto watu wanapewa kipaumbele kwa masomo ya sayansi na teknolojia ili hizo ajira nyingi zibaki nchini, hakuna teknolojia inayo ondoa ajira bila kutengeneza ajira nyingine.
Lakini inategemea hizo kazi nyingi zinamnufaisha nani zaidi. Hata robot anafanya kazi kiwandani lakini anaefaidika ni nani
 
Anamaanisha kwamba ifikapo 2050 baadhi ya ajira zitakuwa zinafanywa na mashine na marobot. Kwa mfano kiwanda kinachoajiri watu 200 kwa sasa kitakuwa kinaajiri watu 25 tuu yaani 175 wanaobaki watakuwa hawana kazi.
Kama maroboti yanafanya kazi ya watu 200 si inatakiwa watu mia mbili wanufaike kwa kupunguza kazi ila mshahara ulele ule. Nini maana ya robot sasa. Si robot anarahisisha kazi
 
Ukionekana unaleta mapinduzi hata yenye faida kwa maslahi ya nchi utawaiwa faster na kuulizwa swali dogo tu "tupe kibali cha wewe kufanya hili", mimi juzi ndiyo nimeanza hata mafanikio bado ila lengo ni kuifaidisha nchi yangu leo unakuja niuliza kibali tena ukiwa na sura ngumu na baadhi kujia na polisi na wanasheria juu wa kuanza kuchambua ibara.

KIBALI
SURA NGUMU
POLISI
KUCHAMBUA IBARA

HAKIKA UMEMALIZA KILA KITU KUHUSU JINSI MIFUMO YETU INAVYOFANYA KAZI
 
Lakini inategemea hizo kazi nyingi zinamnufaisha nani zaidi. Hata robot anafanya kazi kiwandani lakini anaefaidika ni nani
Robot mmoja anaweza ondoa kazi za watu 5 na kuongeza ufanisi ila huyo robot mmoja anatengezwa made watu 50, je hao watu 50 watakuwa Tz au hizo bidhaa zote zitakuwa imported, tusishindane na teknolojia ila tuwe sehemu ya teknolojia.
 
Technology pia inaweza Punguza matumizi ya umeme, wakati tunakua taa za bulb zile zilikuwa zinakula watts 100, Tena hata mwanga vizuri hazina, Sasa hivi unaweza kuwa na Taa mbili sebuleni, tv kubwa, na computer juu zisile huo umeme wa watts 100.

Na technology inakuwa Kwa kasi sana ukitegemea kuja kufundishwa utasubiri sana, watu wajengewe tabia ya kujiongeza wenyewe, elimu isio ya kukariri watu wajifunze kwa kuelewa.
 
Kweli kabisaaaaa
 
Kipindi cha utawala wake hakuliona Hili????????????????
 
Sifa kuu ya kiongozi ni kuonyesha njia kwa waliomtumainia......tunatakiwa kujua serikali imejiandaaje kukabiliana na mabadiliko hayo ya kiteknolojia kisera na kiutendaji.....au 2050 kutakuwa hakuna vijana wa kiTanzania watakaotaka ajira......??
Fact. Viongozi wengi wa Tanzania wana tabia ya kujishangaa wenyewe badala ya kuonesha mwarobaini wa tatizo.
 
Udumavu wa ubongo ni janga zaidi ya teknojia.
Watoto wengi kutokana na udumavu hawawezi kumudu maisha ya kawaida kwa sasa (kadiri ya umri wake), je atafundishwaje ili apambane hiyo 2050 kwenye soko la ajira?
Ajira zitakuwepo kutokana na utashi wa kisiasa. Kwa mfano kutoa motisha kwa wawekezaji wanaotumia nguvu kazi badala ya robot.
Tunahitaji teknolojia na ni muhimu katika elimu, ila tusikurupukie kichwa kichwa.
Tukumbuke hata umeme na maji tu bado vinatutoa jasho kwelikweli!
 
Hujamuelewa mzeeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mzee anamaanisha ukuaji wa Elimu yetu Ni lazima uendane na ukuaji wa Teknolojia. Hivyo vyote vinategemea bajeti imara.

Kama kasi ya ukuaji wa elimu yetu iko nyuma Sana dhidi ya kasi ya ukuaji wa teknolojia Basi wahitimu wa wa kiafrika watapokonywa ajira zao.

Itakapofikia hatua watu walioendelea kutengeneza maroboti madereva, Tiketi kukatwa kwa kadi, huduma kwa wateja Ni roboti, na kila kitu. Sisi Waafrika tutakuwa watazamaji na wahitimu watashindwa kuajirika maana Teknolojia imewatupa mkono kwa sababu hatutaweza kuendesha roboti Wala kuzitengeneza.
 
This is pumbav! Akili inayokuja baada ya kutoka madarakani ni pumbav kabisa! Kikwete angewezaje kuanzisha ufundishaji wa mtandao wakati pesa yote ilikuwa inaibiwa on his watch? Mradi pekee mkubwa ulikuwa ni Mloganzila kwa miaka 10 ya utawala, averaging a total budget of over TZS 170 trilioni in 10 years. Nchi ambayo watu walikuwa wanabeba pesa za escrow yeye anasema siyo za umma, ni za watu binfasi. Hopeless!

Shame upon his shameless face.
 
Hako ka mtu hakastahili hata kusikilizwa. Kama ni theory za uchumi tumeshazisikia sana madarasani kwa walio na uwezo kuliko yeye. Nini anachoweza kutuonesha kuwa ni matokeo ya utawala wake kwa miaka 10?
 
Hako ka mtu hakastahili hata kusikilizwa. Kama ni theory za uchumi tumeshazisikia sana madarasani kwa walio na uwezo kuliko yeye. Nini anachoweza kutuonesha kuwa ni matokeo ya utawala wake kwa miaka 10?
Sasa hivi kuna mabinti wengi sana wanafanya shughuli wasizostahili.

Halafu ukiwaangalia ni mabinti warembo kweli na wamesoma shule za gharama sana.

Mtaji wanaotumia kufanya hizo biashara ni ndogo kuliko hata hizo ADA walizopoteza huko shuleni.

Sasa mtu unabaki unajiuliza maswali tu! Watu kama hawa siwangeenda kusoma shule za kawaida.

Halafu hizo PESA walizopoteza huko wangezitunza kwa ajili ya manufaa ya baadae.
 
Utoaji wa elimu una gharama zake. Kama serikali haiwezi kucover gharama hizo, nchi inakuwa na majengo ya shule na wanafunzi bila kutoa elimu. Gharama kubwa ambayo serikali imejisahau kabisa ni mishahara ya waalimu, badala yake serikali imejaza malipo kwa wabunge na wanasiasa tu, halafu wanakuja kulalamikia elimu.

Mimi nilipokuwa darasa la kwanza Mwalimu mkuu wetu (alikuwa anavaa kaptula nyeupe au khaki, shati nyeupe, tai nyeusi, na stocking nyeupe) alikuwa na gari moja na pikipiki moja. Halafu mwalimu mkuu msaidizi na baadhi ya waalimu waandamizi walikuwa na pikipiki au vespa; vyote vikiwa vimetokana na mishahara yao tu. Leo hii sidhani kama kuna mwalimu anaweza kununua pikipiki ya mchina kwa kutumia mshahara wake tu bila kufanya misheni. Mwalimu anayeingia darasani akiwa na mawazo ya atakula wapi siyo tu kuwa hawezi kuandaa masomo yake vizuri bali pia hawezi kufundisha darasani ila atapiga blah blah ili muda uishe kusudi akafanye mambo yale yanayompa mlo.

Posho za wabunge zinatakiwa zifutwe kabisa zielekezwe kwa waalimu; mbunge akifanya kazi yake analipwa mshahara, siyo alipwe mshahara na posho huku mwalimu halipwi mshahara wa kutosha na wala hana posho yoyote.
 
Elimu haipo ku kufanya uwe Tajiri ama upate ajira nzuri tu,

Anaweza akachonga milango ndio, ila akachonga milango mizuri ambayo mwanzo haikuepo,

Elimu huondoa ujinga na kukupa maarifa mapya, huondoa wasiwasi usio na maana na kukupa maisha yenye Amani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…