Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
huu ni usanii tu wa kiongozi mkuu wa nchi, hakuwa na sababu ya kutoa hii mail address, yeye asubiri tu maswali ya moja kwa moja na sio hadi apewe maswali ayafute mengine ndio aje kutujibu, pia ningependa kumuona mzee mwanakijiji naye akishiriki katika kuuliza maswali pale tbc 1
 
JK kama anataka discussion aanzishe thread humu JF!
Nina uhakika atapata michango iliyotulia kuliko hizo simu atakazokuwa anapigiwa na walewale mabingwa wa kupiga simu kina Manase Muhaha, yule Ustadh wa Tegeta, Chesco mzee wa matunda nk
 
The Farmer;577840]Buchanan, Hakuna sababu yoyote ile ya kupewa maswali in advance. Mambo yanayokera watanzania yanajulikana sitegemei kama kuta kuwa na swali ambali Rais JK atakuwa hajawahi kulisikia.
Ni kweli atakuwa anayajua. Lakini kwa nini sasa ameamua kutupotezea muda eti anataka kuongea live? Anatuzuga au zecomedy nyingine?
Kama kweli hapa rais ameamua kuongea live na wananchi tunatahadharisha tusije kukakosa line kwa sababu ya JAM kwenye mawasiliano...
Kama ulishajaribu kupiga simu kwenye vipindi live vya TV basi hutashangaa. Labda utumie simu ya mmoja wa wasaidizi wake (may be January au Salva) ili akupigie cross. Siyo jam tu, kuna uwezekano mkubwa nyingine zitakuwa "not reachable"! Hii ni Bongo Darisalam ndugu yangu!
 
habari ndio hiyo tukumbuke tuliko toka.....waasisi walikuwa hawasubiri kuongea na watz kwenye tv walikuwa wanawatembelea wananchi huko waliko na kuwasaidia kutatua matatizo yao.Hapa tunazugana tu.Kikwete kaamua kujificha kwenye tv hataki kwenda mbeya anajua hajatekeleza ahadi alizowaahidi hivyo akitia maguu tu wanapopolea mawe msafara wake...........tumepigwa chenga ya mwili hakuna rais wa kwenye tv hapa duniani hizi ni dalili za kuwaogopa wananchi.
Njoo huku kwetu vijijini tukueleze matatizo yetu......

Tutakumbuka enzi za mwalimu.......no kuandaliwa hotuba,hotuba zilitolewa kulingana na hali halisi ya maeneo na matatizo ya wananchi,huto tudakika 90 baada ya miaka4 ya kujinafasi ikulu ndio anataka kutuzuga kwa staili hii
Sidanganyiki...............
 
Naona mmepindisha mada iliyoletwa! Title: 'Kikwete 'Live' TBC1
 
Hivi hamjagundua? Baada ya kuona wamechemsha kwa maamuzi ya NEC Dodoma ya kumbana Spika na kugundua wananchi hawawaungi mkono, wanajaribu kufanya ka utafiti waone je, wananchi maamuzi ya NEC yamewakera kiasi gani? Wanataka kugundua response ya watanzania. HATUDANGANYIKI!!
 
"Kwa maswali ya papo kwa papo kwa rais, naona tunadanganyana, kwa sababu hakuna mtu mwenye uwezo huo wa kukariri kila kitu asubiri tu kuulizwa papo kwa papo kisha ajibu. Tusishangae kusikia majibu mengi yakifanana na "nitafuatilia", "nimekusikia", "sina taarifa", "nasubiri taarifa kutoka kwa wasaidizi" nk. Au aanze kutoa majibu tata kama yale ya Mh Pinda ya kusema "Zanzibar si nchi", au kushabikia uchukuaji wa sheria mkononi (wauaji wa albino).

Kwa nini asijipe nafasi ya kufanyia utafiti maswali hayo, aje na majibu kamilifu kabisa, pengine asubiri tu maswali ya nyongeza ya kutaka ufafanuzi. Hayo ya nyongeza au ya ufafanuzi ndio yawe 'live', na wasaidizi wake wawepo kutoa details, yeye afanye tu kumalizia conclusions na uamuzi, yaani kuyatilia nguvu ya utekelezaji"


BRAVO MUKULU!!!!!
 
Mimi naomba pia Kikwete ajiunge hapa JF ili tumpatie mawazo yetu, wala hatutauliza maswali ila tutampa facts ambazo akizifanyia kazi ataweza hata kuongoza nchi vizuri.
 
Amejiandaa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wananchi? Hofu yangu ni kwamba mengine yanaweza kuwa embarrassing kwa mkuu wa nchi. Hii imekaaje? Au kuna watakaoandaliwa kuuliza maswali?

hilp pia nina wasi wasi nalo, maana jinsi wananchi walivyokuwa na hasira na serikali, sasa sijui itakuwajer. haya wacha tuone hiyo usiku
 
watu wanacholalamika sana ni maswali kwenda yahoo.com
swalikwarais@yahoo.com
je wewe unaona hii ni sawa
kila mtu anataka kumuona raisi akijibu maswali kwa wananchi kwa ajili huo sio utamaduni wa viongozi TZ
 
Kumbe ikulu kuna email hiyo hapo. Kwa isitumike hiyo?????????????????

inawezekana walikuwa hawakumbuki na hapo kutengeneza hiyo ya yahoo ambayo ni bure waweza kuta wameandika na imprest na watasubmit risiti, na kutakuwepo na masalia ya kugawana wao kwa wao
 

Kuna email address kwenye hiyo press release press@ikulu.go.tz, kwa nini hawakutumia hiyo? Au Rweyemamu ana agenda ya siri ku-cook maswali anayotaka yeye kwa raisi !!!
 

msiwena hofu hakuna mtu atakayeweza kumuuliza swali nje ya yaliyopangwa, simu zetu zintkuwa tu zinasema number unayopiga haipatikani kwa sasa....
na ukizingatia wamepewa chance ya kujiingizia mapato leo sina shaka voda na tigo na TTCL hawataacha kurudisha fadhili .
 
Ataongea nini ambacho ni kipya hapa? Kwanza ajiulize yeye mwenye zile ahadi zake alizoahidi amezitimiza? Hali ya nchi ni mbaya and very dissapointing. Juzi kwenye hotuba yake alisema kwamba kuna Uranium imegundulika na kwamba Tanzania itakuwa among 7 countries wanaoproduce Uranium. Ana mpango gani wa kusimamia hii ili isiwe kama madini yetu yanayochimbwa kila kukicha na kuiacha Tanzania bado masikini???? Mheshimiwa Rais anatakiwa kujua kuwa Nchi yake imeshindikana. Tunahitaji muujiza wa Mungu kuweza kuikwamua Tanzania kwenye umasikini.
 
Nina uhakika atapata michango iliyotulia kuliko hizo simu atakazokuwa anapigiwa na walewale mabingwa wa kupiga simu kina Manase Muhaha, yule Ustadh wa Tegeta, Chesco mzee wa matunda nk
ahaa ahaa du! umenikumbusha redio one saa za jioni.
 
.................i'm sorry to say mi nadhani ile michezo ya kuigiza inaendelea. Nothing will come out of this. Maswali yameshapangwa....na majibu tayari yapo.......its really a waste of time to think eti kuna genuine nia ya kusikiliza maoni ya wananchi......BS
 

Nitakuwa busy na big brother huyu muungwana hana kipya!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…