Kikwete 'live' TBC1 Sept 9, 2009

Status
Not open for further replies.
Kwikwikwiiiii mimi nacheka na namna wapigakura wanavyozugwa na mbinu hii....huyu mtu alikimbia mjadala wa wagombea wenziwe alipokuwa anautafuta urais leo eti ndo anaongea 'live' na wananchi?
 
Maswali yatakayoulizwa yatakuwa simpo, ya hovyo na majibu yake yatakuwa miyeyusho. Muungwana hana uwezo wa kujibu maswali magumu yenye maantiki.

Wasomi UDSM walishindwa kumuuliza Mkapa maswali ya maana alipowatembelea Nkurumah. Nahisi hali itakuwa hivyo tu.
 
Jamani leo JK anapanda Kilingeni kupima kama anafaa ama hafai .Maana ameona CCM kwisha habari.

Taarifa ni kwamba maeno mengi ya Jiji hayana umeme. Je watarudisha wakati akiwa hewani? Natafuta habari za mikoani pia kujua kama Umeme una shida kama Dar.

Ila naambiwa Arusha ni giza pia na mida ndiyo hiyo. Inawekana JK akaahirisha maongezi hadi umeme uwepo sote tumsikilize na kumuhoji?
 
 
hakuhitaji kuwaomba wananchi waulize masuali ili ayajibu, kwa mtazamo wangu maisha ya mtanzania wa kawaida toka anapoamka asubuhi mpaka anapoamua kulala usiku ni suali la kutosha ambalo halijapatiwa jibu katika miaka minne ya upangaji wake katika jumba jeupe. Sidhani kama jibu linaweza kupatikana katika dakika 90 za kwnye TV
 
Usijali, maeneo yenye wajuaji wengi umeme utakuwa hamna, maeneo mengine poa tu.

karibu Bongo.

BTW kwanini umeme bongo una mgao usio rasmi, na Tanesco wala hawatangazi?
 
wasi wasi wangu ni kwamba sasa mkakati ndiyo huo maana wanaweza wakamwacha rais apokee simu kitu ambacho sijui , na umeme wameanza kuwakatatisha tamaa watu . Na ikitokea watu wakajanza kwenye bar wakajua basi eneo hilo linakuwa giza zaidi .
 
Imekuaje tatizo la umeme limejitokeza siku rais anataka kusema na watu wake? Ngoja tusubiri, kama hautarudi basi lazima itakuwa ni hujuma ya wale wale tunaowashambulia kila siku - MAFISADI.
 
Dk. iddrisa rashid ni mtuhumiwa, unadhani ataruhusu umeme uwepo?
 
Jamani tuliosafiri kidogo nje ya nchi, tuangalie wapi ? ama tusikilze radio gani Live ?
 

Labda sasa ataweza kujibu swali aliloshindwa kulijibu siku za nyuma nalo ni kwa nini Tanzania ni nchi masikini ?.
 
Kwani wao wajinga, hawataki muone maswali yenu yalivyochujwa. Unadhani atajibu vipi mkataba wa TRL ilhali aliingia yeye! Buzwagi na Richmond Je? Maswali ya mikataba tata, kukumbatia wawekezaji, Nchi kuwa na nchi nyingine ndani ya mipaka yake (UAE) loliondo, maisha bora, rushwa eeeeeeeeeeeeeeeeh! Kizunguzungu
 
Tunaomba links za wale ambao watakuwa LIVE online nasi tuungane na watanzania jamani .
 
wakuu humu jamvini kutakuwa na updates za hotuba yake live?????????????????
 
Maswali yote yatachujwa na kuona ni maswali gani, Labda siku nyingine watabidi waende kati kati ya watu ndio ahojiwe vizuri hakuna jipya hapa zaidi ni zile zile
 
Haya wazee wa nepi ndio tunasogea kumsikiliza kijana nguvu ya ufisadi nchini. Sio mwingine bali ni jemedari kinga ya mafisadi Jakaya M. Kikwete
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…