Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Licha ya tuhuma zilizomzunguka Basil Mramba, Kikwete alimteua kuwa Waziri wake. Licha ya tuhuma zilizomkabili Andrew Chenge, Kikwete alimteua mara mbili kuwa Waziri wake. Kama vile mtu asiyejali tuhuma zinazowakabili watu mbalimbali ndani ya serikali yake (Masha mfano mzuri) Kikwete ameendelea kuwazawadia na kutenda kana kwamba yote yanayozungumzwa yanatokea katika nchi ya kufikirika.
Sasa, mimi ninapendekeza ili yote haya yaishe tujue moja, Rais Kikwete amteue rafiki yake wa karibu na anayesadikiwa kuwa ni mshirika wake pia wa kibiashara na kuwadi wa madeal yake ya kibiashara Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz kuwa Waziri wa Fedha.
Na kama ikiwezekana anaweza kabisa kumpa Uwaziri Mkuu ili yaishe tu. Ni mara ngapi sasa anatuletea watu wale wa karibu ya Vodacom (72 hours) na kuendelea kutuzuga vichwa vyetu. Nianze tena kuhesabu watu wenye mahusiano na Rostam na Vodacom ambao Kikwete amewasogeza karibu na sekta nyeti kana kwamba ndio wale Yesu aliwazungumzia kwenye hotuba ya Mlimani?
I mean, pale aliposema "heri wanaohusiana na Vodacom, maana hao watairithi nchi (Tanzania)"!?
Sasa badala ya kuzugana na kuzungushana ni bora tu waifanye Vodacom kuwa kitengo cha serikali na Rostam kuwa Waziri wa Fedha (au Waziri Mkuu, chochote atachoamua RA).
Mwanzoni alipoingia madarakani tetesi zilikuwepo kuwa RA angeweza kupewa Uwaziri lakini yeye mwenyewe RA (au kwa ushauri wa wengine) ali decline. Sasa kwa vile muhula wa kwanza ndio huo unakwisha, ni bora kumpa Uwaziri wa Fedha.
May be not, Nadhani ampe Uwaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Labda hiyo siyo nzuri sana. Pengine Uwaziri wa Biashara na Mipango. Siyo hilo? Vipi kuhusu Uwaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora)?
Vyovyote vile, mimi nakupigia magoti mheshimiwa Rais mpe Uwaziri Rostam ili hatimaye binafsi nijue umeamua kututukana kwa jumla Watanzania kuliko huu mtindo wa reja reja. Mpe tu, tena ukipenda unaweza kumtengenezea cheo cha "Naibu Rais" or something flashy like "Deputy Prime Minister and Minister of Finance and Special Advisor to the President on Economic Affairs with Special Portfolios"!