Kikwete: Mwaka 95 walinishauri tuunde chama, nikawaambia hatutakuwa registered na Serikali

Kikwete: Mwaka 95 walinishauri tuunde chama, nikawaambia hatutakuwa registered na Serikali

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Rais wa awamu ya nne leo akiongea na kituo cha redio cha Clouds FM kwenye kutimiza miaka 72 tangu aje duniani, ameongelea uchaguzi wa ndani ya chama cha CCM mwaka 1995.

Kikwete amesema baada ya Benjamin Mkapa kuteuliwa na CCM, watu waliokuwa upande wa Jakaya Kikwete walipandwa na Jazba akiwemo mama Anna Makinda ambae alidai angelikuwepo mgombea binafsi basi wangemuunga mkono JK kuwania nafasi hiyo.

Kikwete amesema wapo waliotaka wakasajili chama kipya ili JK apeperushe bendera.

Kikwete aliwaambia 'calm down' kwani 'advantage waliyonayo umri wake bado unaruhusu kwani alikuwa na miaka 45 muda ule na miaka kumi inayofata angekuwa na 55 sawasawa na umri aliokuwa nao Mkapa 1995.

Kikwete amesema alipoomba kuzungumza kwenye mkutano wa CCM, walipata hofu.
 
Bora angezungumzia udhaifu wake ktk urais badala ya kutueleza mambo ambayo ni past tense. Yana faida gani kwetu? Hicho ni chama chao na ufisadi wao na unafiki wao.
 
Hata makundi ndani ya CCM ndiyo yatajayoimaliza chama chenyewe.
 
Dah ile hotuba siku ile pale Dodoma ilimfanya Mwalimu Nyerere asimame na kupiga makofi peke yake pale meza kuu.

Ile Hotuba ilimfanya Nyerere aamini Kijana wake kaiva sasa, Nyerere ni moja ya watu waliokuwa wanampenda sana JK (usiniulize kwa nini). Japo JK aliamini Mzee alimnyima dodo pale Dom na in his 45yrs angeweza kuwa Jengo jeupe naamini mpaka leo ana kinyongo kwa kupunguziwa muda wa bata.

Marehemu Seif Sharrif na JK ni moja ya vijana ambao Nyerere aliwakuza na kuamini siku moja watakuja kuwa viongozi wakubwa, shida ya Seif kwa mzee ni utata na uhafidhina, na shida ya JK kwa mzee ilikuwa ni uchekibob na usaigon.
 
Bora angezungumzia udhaifu wake ktk urais badala ya kutueleza mambo ambayo ni past tense. Yana faida gani kwetu? Hicho ni chama chao na ufisadi wao na unafiki wao.
Sasa akizungumzia udhaifu wake itakusaidia nn? Urais wake ulishapita mkuu
 
JK na SIX waliutengeneza mtandao, na JK huyo huyo akauua mtandao baada ya kutaka kumzidi nguvu, JK anakipaji cha kuchanga karata na kuzicheza akisaidiwa na kuwa kwake mtoto wa town.

Alimuingiza mjini SIX na UPM akajaa, akapozwa na Uspika akapoa, SIX akatumika kama fimbo kumchapa nywele nyeupe kupitia vijana wake pale bungeni na usajili mpya kutoka kyela, white hair akakaa huku backup yake ya burushi wa Igunga ikipigwa pin.

Mungu akurehemu huko uliko SIX vijana wako yule wa kigoma na mwingine wa koromije wapo wanaendeleza kazi uliyowafundisha japo mmoja kakengeuka na hata kumgeuka yule uliyeomba awe mentor wake matokeo yake akadandia mtumbwi uliozama ziwani.
 
Dah ile hotuba siku ile pale Dodoma ilimfanya Mwalimu Nyerere asimame na kupiga makofi peke yake pale meza kuu.

Ile Hotuba ilimfanya Nyerere aamini Kijana wake kaiva sasa, Nyerere ni moja ya watu waliokuwa wanampenda sana JK (usiniulize kwa nini). Japo JK aliamini Mzee alimnyima dodo pale Dom na in his 45yrs angeweza kuwa Jengo jeupe naamini mpaka leo ana kinyongo kwa kupunguziwa muda wa bata.

Marehemu Seif Sharrif na JK ni moja ya vijana ambao Nyerere aliwakuza na kuamini siku moja watakuja kuwa viongozi wakubwa, shida ya Seif kwa mzee ni utata na uhafidhina, na shida ya JK kwa mzee ilikuwa ni uchekibob na usaigon.
😂😂😂Safi sana nakubali mkuu
 
Back
Top Bottom