Kikwete Political Economist

Kikwete Political Economist

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Kikwete ndiyo binadamu anayejua uchumi na siasa kwa pamoja. Agenda yake ya awamu ya pili alifanikiwa sana. Aliunganisha makao makuu ya mikoa kwa barabara za lami, nchi za jirani kwa lami, mfano mpaka wa Sirari, Tarakea, Holili, Hororo. Mtu mwingine anayejua uongozi Anna Semamba Makinda.

Nimependa uchambuzi wake wa sensa ya 2022 kuwa population ya Dar imeshuka kutoka 10% mpaka 8%. Sababu ujenzi wa miundo mbinu mikoani. Km ningeweza kumshauri Rais wangu mama unganisha mikoa kwa lami 2032 population ya Dar itakuwa chini ya 5%.

Umeme umeenda sehemu nyingi kijiini. Unganisha kwa mfano Arusha-manyara-Dodoma kupitia Simanjiro- Kiteto-Kongwa. Unganisha Tanga-Manyara-Dodoma-Singida kupitia Handeni-Kiteto-Kondoa-Hanang-Singida.

Unganisha mikoa ya Arusha-Manyara-Singida-Simiyu kupitia Karatu-Mbulu-Sibiti-Mwanhuzi-Lalago-Maswa. Barabara ya kuunganisha mikoa ya Morogoro-Njombe-Mbeya. Rais wetu tunakuombea tukijua una miradi mikubwa ya kukamilisha. Haya yawe agenda yako ya 2025. Heri ya mwaka mpya 2023!
 
Akiendelea KUKOPA ili aunganishe hizo barabara asilaumiwe.

Maana watu wanashauri vizur yaan ila tukija kwenye utekekelezaji wa mawazo yao kupitia loan tozo na levy utasikia yowe lake.

Sisi tunatembea kifua mbele na mama SSH
Happy Mapinduzi Day
 
Umeona ehh. Na kule wamekukwoti nje ya maudhui... Usikwazike Mkuu nilipata kichechemeo kwenye tarakilishi.

Lock step!
Hilo jamvi hili!

Ukiona wanakusema vizuri vizuri kama nyerere,shtuka Sana!

Wanakuwangia hao!

Binadamu hasemwi vizuri akiwa hai,mara nyingi wanahofia usije ukawafunika,lakini ukiwa umelala unono Basi utasemwa vizuri mpaka Basi!

Mungu ibariki Tanzania nchi yetu niipendayo Sana
 
Nimependa uchambuzi wake wa sensa ya 2022 kuwa population ya Dar imeshuka kutoka 10% mpaka 8%. Sababu ujenzi wa miundo mbinu mikoani. Km ningeweza kumshauri Rais wangu mama unganisha mikoa kwa lami 2032 population ya Dar itakuwa chini ya 5%.
Kuna ukweli ktk hili. Siku hizi vijijini kama mjini tu.
 
Back
Top Bottom