Kikwete, tafadhali fuata nyayo za Pervez Musharraf

Kikwete, tafadhali fuata nyayo za Pervez Musharraf

Lakini angekuwa JKN msingeweza hata kuandika hivi tunavyoandika! Kulikwa hamna uhuru wa vyombo vya habari na hamna uhuru wa mawazo. Shukuruni JK ameruhusu hili.

Duh, Mr Spin doctor! Kweli unalipwa kwa haki maana unajitahidi sana kutafuta positive angle lakini naomba kumtaarifu mh Msanii aka Vasco Da Gama na timu yake kwamba hotuba ya leo imemvua nguo uchi wa mnyama kwa vile ameonyesha madudu yote aliyokuwa anayatenda miaka yote hii. Watanzania tumefunguka macho. Hawezi kutudanganya kijinga hivyo. Asisubiri mpaka atimuliwe, aondoke kwa hiari.
 
Kwa kifupi rais hatuna. Lakini tunashukuru mungu leo ndio tumejua hasa yuko upande gani
 
Kumbe ukitaka kuiba basi iba pesa ya kubwa na ya kutisha. Serikali inakupa muda wa kurudisha huku ikikubembeleza.

Lakini ole wako ukiiba pesa mbuzi ama uwe mwizi wa mifukoni, ni jela ama kifo.

Hakuna ubishi JK ni msanii na hafai kuwa Raisi wa nchi. Bora kuzaliwa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa Mtanzania na kudhulumiwa haki yako na mafisadi ambayo Raisi anayatetea.
 
Wito wangu kumuomba Kikwete aingie mitini hautokani na hotuba ya jana pekee wala si kutokana na matokeo ya hamaki ya watu kutokana na hotuba hiyo.

Naomba mrejee tangu kule kwenye Screw Muungwana, Thank God for giving us Kikwete, Kikwete is hopeless na nyingine nyingi, kila kitu ilikuwa ni wimbo kumuomba huyu bwana ama afanye kazi au aachie kazi wenye uwezo wafanye!

Nikafikia hata mahali nikasema Utawala wake in batili "illegitimate kingdom" bado anaendelea kuonywsha kuwa nimekuwa sahihi kwa 80%!

Nyerere alipoona mambo ni mazito na hakuna mwenye kutaka msikiliza alilinusuru Taifa na kung'atuka huku akiheshimiwa. Hali mbaya baada ya uchaguzi 1980, ilikuw ani tosha sana kwa mtu mwenye busara kuona mbali na hivyo kutoa nafasi kwa nguvu na sauti mpya kuongoza merikebu.

Kikwete kwa miaka karibu mitatu, amechuja ile hotuba yake ya Kwanza kiasi kuwa hata ile hotuba haina maana tena.

Mbaya zaidi ni kuendelea kukumbatiana na wanaodaiwa kuwa ndiyo wenye CCM!

Nampa ushauri na kutumia kauli za mhafidhina kuwa atumie Busara na Hekima abwage manyanga aingie mitini!
 
Kumbe ukitaka kuiba basi iba pesa ya kubwa na ya kutisha. Serikali inakupa muda wa kurudisha huku ikikubembeleza.

Lakini ole wako ukiiba pesa mbuzi ama uwe mwizi wa mifukoni, ni jela ama kifo.

Hakuna ubishi JK ni msanii na hafai kuwa Raisi wa nchi. Bora kuzaliwa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa Mtanzania na kudhulumiwa haki yako na mafisadi ambayo Raisi anayatetea.

Mimi kama ni mhalifu Tanzania, nitakata rufaa na kutaka kesi ifutwe au nipewe muda nirudishe mali na nisamehewe, maana tayari mfano hai ambao unalindwa na Serikali na mamlaka yake umeonekana "waliohujumu na kuliibia Taifa Benki kuu wamepewa muda kurudisha fedha la sivyo watafunguliwa mashtaka'!
 
Back
Top Bottom