Wito wangu kumuomba Kikwete aingie mitini hautokani na hotuba ya jana pekee wala si kutokana na matokeo ya hamaki ya watu kutokana na hotuba hiyo.
Naomba mrejee tangu kule kwenye Screw Muungwana, Thank God for giving us Kikwete, Kikwete is hopeless na nyingine nyingi, kila kitu ilikuwa ni wimbo kumuomba huyu bwana ama afanye kazi au aachie kazi wenye uwezo wafanye!
Nikafikia hata mahali nikasema Utawala wake in batili "illegitimate kingdom" bado anaendelea kuonywsha kuwa nimekuwa sahihi kwa 80%!
Nyerere alipoona mambo ni mazito na hakuna mwenye kutaka msikiliza alilinusuru Taifa na kung'atuka huku akiheshimiwa. Hali mbaya baada ya uchaguzi 1980, ilikuw ani tosha sana kwa mtu mwenye busara kuona mbali na hivyo kutoa nafasi kwa nguvu na sauti mpya kuongoza merikebu.
Kikwete kwa miaka karibu mitatu, amechuja ile hotuba yake ya Kwanza kiasi kuwa hata ile hotuba haina maana tena.
Mbaya zaidi ni kuendelea kukumbatiana na wanaodaiwa kuwa ndiyo wenye CCM!
Nampa ushauri na kutumia kauli za mhafidhina kuwa atumie Busara na Hekima abwage manyanga aingie mitini!