SHUPAZA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2009
- 562
- 23
Na Sadick Mtulya
RAIS Jakaya Kikwete jana alirejea nchini akitokea Cuba na kujibu mapigo ya makada mbalimbali wa CCM wanaomtuhumu kushindwa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema anajipanga kujibu tuhuma dhidi yake kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu ambazo zilitolewa na makada mbalimbali wa CCM, wakiwemo mawaziri wa zamani.
Lakini Kikwete alidokeza majibu yake kwa kusema: "Japokuwa ndio kwanza ninafika, sishangazwi na yote mabaya yaliyozungumzwa dhidi yangu katika kongamano hilo. Ningeshangazwa kama ningesemwa vizuri."
Jakaya, ambaye alikuwa anarejea kutoka ziara ya takribani wiki mbili kwenye nchi za Jamaica, Cuba na Trinidad na Tabago ambako alihudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, alisema hatishwi na maneno yaliyozungumzwa kwa kuwa watu waliozungumza wanajulikana wanatoka upande gani.
Katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Rais Kikwete alishutumiwa kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na kukiacha chama kikipoteza mwelekeo na kutekwa na matajiri wachache.
"Japo bado sijapata taarifa vizuri kuhusu yote yaliyozungumzwa katika kongamano hilo; siwezi kushangazwa sana, lakini ninakwenda kupata taarifa kamili na kujadiliana na wenzangu kisha nitajibu mambo yote yaliyokuwa na maana na yale ambayo hayana maana na yaliyosemwa kwa chuki, tutayapuuza tu," alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema hashangazwi na hali iliyotekea kwa kuwa binadamu wanatofautiana kimtazamo, lakini akasisitiza kuwa anachojali zaidi ni dhamana aliyonayo kwa umma.
"Kama nilivyosema kuwa nimedokezwa kidogo tu, lakini naomba muelewe kuwa huwezi ukamridhisha kila mtu kwani binadamu wamegawanyika katika sehemu tatu," alisema.
"Asilimia 15 watakupenda, asilimia 15 nyingine watakuchukia na asilimia 70 iliyobaki watabaki wanaangalia upepo unaelekea wapi hivyo tusubiri kuna maamuzi tutafanya," alisema Rais Kikwete.
Katika mkutano huo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, waziri wa zamani wa menejimenti ya utumishi wa umma, Matheo Qares alisema iwapo rais atashindwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi kabla ya 2010, CCM haina budi kumtosa na kumteua mgombea mwingine wa urais.
Naye waziri wa zamani kwenye serikali ya awamu ya pili, Mussa Nkangaa alisema CCM sasa imetekwa na wafanyabiashara matajiri na kuachana na sera zake za kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, ndio maana imekuwa vigumu kushughulikia mafisadi.
Katibu mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula, katika mahojiano na Mwananchi, alisema tatizo la kupeana uongozi kwa urafiki limefanya taifa liwe na viongozi wasio na sifa na kusababisha mambo yanayoendelea kutokea sasa ndani ya chama hicho kikongwe.
CCM inaonekana kuwa katika hatari ya kuparaganyika kutokana na kuwa na makundi ambayo yanarushiana tuhuma kila kukicha. Tuhuma hizo zimekuwa zikitolewa kwenye mikutano ya Bunge na hivi karibuni zilihamia kwenye kikao cha Halmashauri Kuu na baadaye mkutano wa kamati iliyoundwa kuchunguza mfarakano huo, maarufu kama Kamati ya Mwinyi na wabunge kilichofanyika Dodoma.
Kikwete, ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa kufanya safari nyingi za nje zinazokula fedha za walipa kodi na huku akishindwa kutulia nyumbani kutatua matatizo mengi yanayoikabili nchi kwa sasa, alitetea safari hizo akisema ni vigumu kwake kuacha safari hizo kwa kuwa hazina mbadala.
Na kuonyesha kuwa hawezi kuziacha, Kikwete akaongeza:"Na wiki chache zijazo ninatarajia kwenda nchini Denmark kuhudhuria mkutano wa Capenhagen."
Ikulu pia iliwahi kutoa taarifa ya kutetea ziara hizo ikisema kuwa zina manufaa kwa nchi kwa kuwa Rais Kikwete huenda nje kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo. Ikulu ilitoa kauli hiyo baada ya wananchi kulalamika kuwa fedha nyingi hutumika kwenye safari hizo.
Kikwete anatarajia kuongoza msafara wa watu takribani 60 atakapokwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Kuhusu hali ya afya yake, Kikwete, ambaye alizidiwa nguvu jukwaani mjini Mwanza kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kufanya safari ndefu bila ya kupumzika, alisema yuko salama lakini anatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya.
"Nilipokuwa huko nilipima afya yangu na hasa akili na mishipa ya damu na wataalamu wakaniambia nipo salama. Ninatarajia kupumzika baada ya mwaka mpya," alisema Kikwete. Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa hali yake ni salama wataalamu wamemshauri kupunguza ratiba za kazi za kila siku.