Kikwete Vs Hayati Magufuli: Magufuli yuko sahihi kuhusu Katiba Mpya

Kikwete Vs Hayati Magufuli: Magufuli yuko sahihi kuhusu Katiba Mpya

Wildlifer

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2021
Posts
1,884
Reaction score
5,235
Salam!

Wote tunajua mchakato wa kuandika Katiba mpya Tanzania wakati wa Kikwete na hadi kukwama kwake.

Wote tunajua msimamo wa Magufuli wa kutokutaka kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Sasa Rais Hassan ameanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Mimi ni Realist. Na napenda tuwe realist katika kuitazama katiba mpya na mchakato wake.

Wanachokitaka Upinzani ni Mfumo huru wa kidemokrasia na kisiasa ambao utawaondoa CCM madarakani. CCM (hata wangekuwa Chadema kwenye nafasi hii), wasingekubali. Ndio ambacho CCM haikikubali kwa Kikwete. Na mchakato ukafeli.

Wanadamu tuna hulka mbili za kudeal na mambo. Za kona kona na moja kwa moja.

CCM hawawezi kukubali kubadili katiba hii kwani ndio inawaweka madarakani. Magufuli alikuwa mkweli tu, mchakato ni kupoteza pesa bure za Watz na hatutafikia mahala pa maana.

Mwisho wa Siku, mtazamo wa Magufuli ndio utakuwa sahihi kwenye mchakato huu.. REALISM.
 
Mkwamo wa Katiba ya Warioba ukiisha ujue barabara ya Nyakanazi-Kigoma itatoka kwenye mkwamo pia.
 
Wenye nchi walishasema “Kitabu kilichoandikwa kisha kikaachwa kitamalizwa katika hesabu hii “ halafu wewe wildfire wa Sigimbi unaleta mambo ya Realism ivi una akili wewe ?
 
Je, Katiba iliyopo ina mapungufu gani ya msingi, ya kisiasa au/na kidemokrasia (Uhuru na Haki) au tatizo ni tafsiri yake kwa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu?
 
..iandikwe katiba inayotoa HAKI SAWA kwa Watanzania wote.

..Maslahi ya vyama vyote yatakuwa salama kama tukiandika Katiba inayotulinda Watanzania wote.
 
Kinaniuma sio CCM kutoruhusu Katiba Mpya, bali ni kuchezea hela kwa mchakato ambao tunajua hauzai matunda.
Wanajitafutia ulaji tu huku wanaumiza wananchi kwa kuongeza TOZO ; Wakati huo huo wananchi wanaumizwa na mfumuko wa bei!!
 
Mkwamo wa Katiba ya Warioba ukiisha ujue barabara ya Nyakanazi-Kigoma itatoka kwenye mkwamo pia.
bwashe mbona hiyo barabara inakaribia kwisha?mara ya mwisho ulipita lini?tunaosafiri na hiyo njia tunaijua vizuri.
 
Salam!

Wote tunajua mchakato wa kuandika Katiba mpya Tanzania wakati wa Kikwete na hadi kukwama kwake.

Wote tunajua msimamo wa Magufuli wa kutokutaka kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Sasa Rais Hassan ameanzisha mchakato wa Katiba Mpya.

Mimi ni Realist. Na napenda tuwe realist katika kuitazama katiba mpya na mchakato wake.

Wanachokitaka Upinzani ni Mfumo huru wa kidemokrasia na kisiasa ambao utawaondoa CCM madarakani. CCM (hata wangekuwa Chadema kwenye nafasi hii), wasingekubali. Ndio ambacho CCM haikikubali kwa Kikwete. Na mchakato ukafeli.

Wanadamu tuna hulka mbili za kudeal na mambo. Za kona kona na moja kwa moja.

CCM hawawezi kukubali kubadili katiba hii kwani ndio inawaweka madarakani. Magufuli alikuwa mkweli tu, mchakato ni kupoteza pesa bure za Watz na hatutafikia mahala pa maana.

Mwisho wa Siku, mtazamo wa Magufuli ndio utakuwa sahihi kwenye mchakato huu.. REALISM.
Mkuu, asante kwa mada; ila nitakupinga kwa sababu you sound more of defeatism and pessimism leaning.

Nani alikudanganya kuwa CCM wanahodhi au wataendelea kuhodhi au kuchezea mustakabali wetu na wa Taifa kiujanja ujanja miaka ijayo? HAPANA.

Narudia, si kweli. Hata wao CCM wanalijua hilo.

Kuna njia na sababu nyingi za kwa nini hauko sahihi, na CCM watashindwa kuwa ulichokisema; briefly:-

1. Demography ya nchi yetu

2. Dynamics za siasa zetu - kuna fukuto linatengeneza momentum, mithili ya wimbi la bahari hivi, hilo litabadili siasa zetu (CCM watake wasitake). Yaani siasa zetu zitakuwa tofauti sana ndani ya miaka 10-15 ijayo. Stay tuned.

3. Elimu na national maturity level- kama jamii na Taifa, kuna level ya elimu na maturity tutaifikia (naturally or otherwise) ambayo nayo itabadili kabisa uwanja, kanuni na matokeo ya mchezo.

4. Dunia na mambo ya kimataifa, kiuchumi na kisera.

5. Mwenyezi MUNGU.
 
Je, Katiba iliyopo ina mapungufu gani ya msingi, ya kisiasa au/na kidemokrasia (Uhuru na Haki) au tatizo ni tafsiri yake kwa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu?
Mapungufu yake mengi na makubwa sana. Yamaeshajadiliwa mno kwa urefu zaidi ya miaka 30 sasa. Hivyo sio rahisi kuyaweka hapa (tedious).

Ushauri wangu fanya utafute ripoti ya Tume ya Rais ya Jaji Nyalali uanzie pale.
 
Back
Top Bottom