JK akizungumza kwny mkutano wa kamati ya amani ya DSM alielezea kusikitiwa, kuhuzunishwa na kufadhahishwa na tamko la TCF la kuipinga katiba pendekezwa na m/kadhi. Kwa kwel wanaCCM wanatatizo kubwa sana la 'double standard' na kuwadhani wananchi hawaelewi kiasi cha kuwa zuzu.
Je ni nani mwanzilishi wa kutumia taasisi dini kukataa katiba pendekezwa?
Waanzilishi ni waliokua wakilishi wa jumuiya za Kiislam na baadhi ya waumini wao kwny BMK walipoazimia kuikataa "kijarida cha Chenge" kama serikali haitaridhia m/Kadhi. Waliweka msimamo wao wazi watapiga kura ya hapana ikiwe m/Kadhi haitakuwepo. Cha kusikitisha si WM Pinda wala Serikali yake wala CCM waliong'aka. Je iweje nongwa ikiwa TCF wakihamasisha kura ya hapana?
Nn CCM wanachokosea?
Serikali ya CCM inataka kujinufaisha kisiasa zaidi kwa kutumia masuala ya kidini huku JK akijua na kukiri fika hali ya amani iko shakani na taifa liko majaribuni. Wanajua fika na tena pasi na shaka dawa ilikwishapatikana tena kitambo nayo ni rasimu ya Warioba(Rasimu ya tume ya mabadiliko ya Katiba).
Nn mapendekezo yangu?
Taifa tuachane na mambo ya dini kama ilivyoshauri kamati ya Warioba. Kama taifa tujikite kwenye ujenzi wa taifa letu maskini na linalokabiliwa na changamoto nyingi pamoja na maadui umaskini, ufisadi, maradhi,ujinga na utumiaji mbaya wa madaraka.
Hitimisho. Amani iliyopo itaendelea kuwepo isipokua tu kwa uzembe na maksudi ya serikali ya CCM kulinda maslahi na washirika wao bila kujali mustakabali na maslahi mapana zaidi ya taifa. Tusisahau pasipokua na haki hakuna amani
Wasalaam!