Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Kikwete: Wapinzani ndio wanaochochea vita dhidi ya Malawi

Status
Not open for further replies.
WHAT? I wish ningesikia hiyo BBC kwa sikio langu. Mimi ni Tomaso siamini. Kama ni kweli JK kasema hivyo, nadhani alikuwa anatania ili watu wapandishe munkali.
 
Nieesikia BBC leo asubuhi, na wamemnukuu Rais wetu akiwa Msumbiji akisema kuwa Tanzania haina mpango na vita dhidi ya Malawi, bali vinachochewa na viongozi wa vyama vya upinzani wenye uchu wa madaraka. Nilikuwa sina access na habari juu ya mwendelezo wa mgogoro huu tangu mwanzo. Niliowasikia ni kina Lowasa, Sitta na Membe. Imekaaje hii, hawa ni wapinzani siku hizi? Au?
 
kuna thread inajadili hili tngu asubuhi ...futa hii ufatile ile....
 
Rais wa nchi kuongelea upinzani negatively akiwa ugenini (nje ya nchi) ni jambo linalomdharirisha hata yeye mwenyewe. Kiongozi makini hawezi kufanya hivyo.
 

He must have been overwhelmed by something and went off his mind. Tumweleweje mbona huo ni uongo mweupe? Waliodai vita ni wana CCM (Lowassa, Sita and Mwmbe), wapinzani wanaamini nguvu ya diplomasia sasa haya kayatoa wapi mbona anawageuzia wapinzani kibao? What happens to the president when he lies?
 
Jk kuwa madarakani ni kama mzigo wa mwizi kwa watz, hata kama umechoka hakuna wa kukusaidia
 
Bw. Nikupateje tatizo letu Wabongo hatuna tabia ya kufuatilia mambo na kuya analyse bali sisi huwa tunaenda na matukio. Asilimia kubwa ya ramani za kimataifa ambazo ziko neutral (ukiachilia mbali zilizochapwa TZ au Malawi) zinaonyesha mpaka haupo katikati bali ni shoreline upande wa TZ lakini wengi wetu hili hatulijui na wala hatuna muda wa kufuatilia. Kama kweli tuna dai portion ya hili ziwa basi tujenge hoja na strong basis for claims sio kubwabwaja maneno mengi bila ya ya uchambuzi makini maana mpaka hapa rais kashaonesho udhaifu tulionao kwa upande wa hoja tayari.
 
Inasikitisha sana tunapokua na Raisi Mwongo na asiyejiamini.Sote tulisikia kauli za Membe na Lowasa, tukasikia pia kauli za upinzani toka kwa Prof Safari,Baregu na Lipumba.Je! Ni wepi hapo walokua wakihimiza vita? Au ndio yale anapewa taarifa potofu? Mie binafsi naona aibu kuwa na Rais wa namna hii

Ni aibu sana niko ughaibuni natamani niote mbawa nije kujificha ktk misitu ya kwetu!!!!!!!! Taarifa potofu kila anaposema kinyume na inavyopasa yeye hana akili? Kama ndivyo basi watanzania tunashida sana kuongozwa na mtu wa aina hii.
uyu
 
Unajua Malawi ni kipenzi cha nchi za magharibi hasa baada ya kukubali ndoa za jinsia moja, Sasa JK amesoma alama za nyakati, vita dhidi ya Malawi itakuwa ni vita dhidi ya Uingereza na Marekani. Amestuka msanii.
 
Mkuu Emeka Anyaoku

Source , linki, tarehe ya ripoti
ni muhimu wana-jamiiforum ili tujadili bila chenga wala nini na kuifanya JamiiForums source ya kuaminiwa tuwe zaidi ya Global.
 
Mie wakati mwingine huwa nasita kumtaja huyu Rais wetu wa sasa kwa initials zake eti "JK" maana wakati mwingine huwa nahisi watu wanamtaja Julius Kambarage!

Ila kwa statement ile nahisi mazungumzo yao yalikuwa faragha sana, na inawezekana first lady Mama Riz1 hakuwepo around, au rais wetu alikuwa anaomba uzazi kwenye hayo mazungumzo badala yake anatoa a weak statement!
 
Ni CDM tu hao ndio maana wakasema
liwalo na liwe, wakasema hawataki kura za wafanyakazi, wakasema wanafunzi wanapewa mimba kwa kiherehere chao, wakasema hawajui kwanini tz ni masikini, na hawakuishia hapo wakasema wafanyakazi wakigoma au kuandamana watashuhulikiwa na ikibidi wagawane majengo ya serikali yani moi muimbili na kwa kova central au segerea Chadema Wana chafua Hali ya ccm hawana Hata huruma Dah
 
me nilisikia kwa membe na LOWASSA hivi hawa ni WAPINZANI?:israel:
 
Hivi ni kweli kasema wapinzani ndio wanachochea vita? Kama ni kweli basi ni kituko cha mwaka.
 
Source: BBC

...anasema viongozi wa upinzani ndio wanaoongelea maswala ya vita dhidi ya wanyasa concern mgogoro.

AMESEMA KATU TANZANIA HAITAPIGANA NA MALAWI.

My take:
Lowassa, Membe, Sitta ni Wapinzani?

Kasema UPINZANI au VYAMA VYA UPINZANI? Inabidi tutofautishe hayo maneno.
 
Hivi kikwete ana akili sawa kweli, yaani amiri jeshi mkuu, ambaye yupo juu ya mkuu wa majeshi anatoa kauli tata kama hiyo? Kwa maneno hayo CDF aondoe askari wake mpakani na malawi. kweli tuna rais kilaza kuliko wote afrika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom