Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,199
Inashangaza sana, na inasikitisha sana kwamba Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete, anayeamini katika mazungumzo zaidi kuliko nguvu, ameingia kwenye mkumbo uleule wa kufanya yaleyale ambayo amemshauri mwenzake Kagame aachane nayo.
Hivi kulikuwa na mantiki gani kwa Kikwete kuutangazia umma tofauti zake na Kagame ilihali anaamini katika kumaliza migogoro kwa mazungumzo? Hivi Kikwete haijui namba ya simu ya Kagame? Kwanini hajampigia simu Kagame ili wayamalize, kabla ya kutuhutubia sisi? Au kama anaona hataweza kuongea na Kagame moja kwa moja, ina maana haijui namba ya Mseveni au ya Uhuru? Ameshindwa nini kuwaomba hawa majirani wamuitie Kagame ili wapatanishwe?
Japo amejibu vema katika hotuba yake lakini maneno yake mbele ya mtusi yule yanaweza kuongeza chuki badala ya kumaliza hizo tofauti. Baada ya kutoa hotuba ile, Kikwete anadhani atakuwa amesaidiaje kumaliza tofauti zake na Kagame? Je wanaweza sasa kukaa chini na kuyamaliza kwa vile tu amesema anasikitishwa na kauli za Kagame?
Dalili zinaonyesha kwamba Kikwete ameanza kutengwa na marais wengine wa Africa mashariki. Ni dhahiri Rais wetu ni tatizo, inawezekana anaiponza nchi. Haiwezekani kwamba ushauri tu dhidi ya Kagame ndiyo uliosababisha haya yote. Lazima kuna mengine nyuma ya pazia, ambayo Kikwete hataki kuyaweka wazi.
Kwa hakika kama Kikwete anaamini katika mazungumzo tunamwomba basi atafute muafaka na Kagame kwa njia ya mazungumzo badala ya kuendelea kurushiana maneno kupitia kwenye mikutano na hotuba. Maana naamini baada ya haya, Kagame naye atajibu! What will be next. Watanzania hatutaki vita sasa hivi. Muyamalize kama mlivyoyaanzisha.