Kikwete, zungumza na Kagame!!

Kikwete, zungumza na Kagame!!

kwa nini isiwe Kagme aongee na Kikwete ila kKikwete aongee na Kagame hii haiwezekani Kagame kama ni mwanamme ushauri aliopewa angejibu palepale asingesubiri akacheze zeze nyumbani kwake tena kwa kutoa maneno ya kejeli na matusi pamoja na kutumia vyombo mbalimbali vya habari kumkashifu raisi wetu. Hicho alichofanya Kagame kinadhihirisha kuwa ni mwoga na mnafiki anayependa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Huku akiitumia Genocide aliyoianzisha mwenyewe kama chambo.

Kagame ndio anapaswa aongee na Kikwete maana yeye ndiye kaanzisha ugonvi wa mawe kwenye nyumba ya vioo.

Mkuu hoja ya kumaliza tofauti kwa mazungumzo ni ya kikwete, siyo ya kagame.

Ni bora huyu kikwete ambaye ni muumini wa sera ya majadiliano mezani aiitekeleze sera anayoisadiki kwavitendo.

Ameshindwa kuitekeleza kwa walimu, madaktari, wahanga wa mtwara, Arusha na mwanza, basi hata huko alikotoa

ushauri ameshindwa? Je tuamini kwamba kweni anaamini katika majadiliano? au anaamini katika propaganda na mipasho?
 
Inashangaza sana, na inasikitisha sana kwamba Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete, anayeamini katika mazungumzo zaidi kuliko nguvu, ameingia kwenye mkumbo uleule wa kufanya yaleyale ambayo amemshauri mwenzake Kagame aachane nayo.

Hivi kulikuwa na mantiki gani kwa Kikwete kuutangazia umma tofauti zake na Kagame ilihali anaamini katika kumaliza migogoro kwa mazungumzo? Hivi Kikwete haijui namba ya simu ya Kagame? Kwanini hajampigia simu Kagame ili wayamalize, kabla ya kutuhutubia sisi? Au kama anaona hataweza kuongea na Kagame moja kwa moja, ina maana haijui namba ya Mseveni au ya Uhuru? Ameshindwa nini kuwaomba hawa majirani wamuitie Kagame ili wapatanishwe?

Japo amejibu vema katika hotuba yake lakini maneno yake mbele ya mtusi yule yanaweza kuongeza chuki badala ya kumaliza hizo tofauti. Baada ya kutoa hotuba ile, Kikwete anadhani atakuwa amesaidiaje kumaliza tofauti zake na Kagame? Je wanaweza sasa kukaa chini na kuyamaliza kwa vile tu amesema anasikitishwa na kauli za Kagame?

Dalili zinaonyesha kwamba Kikwete ameanza kutengwa na marais wengine wa Africa mashariki. Ni dhahiri Rais wetu ni tatizo, inawezekana anaiponza nchi. Haiwezekani kwamba ushauri tu dhidi ya Kagame ndiyo uliosababisha haya yote. Lazima kuna mengine nyuma ya pazia, ambayo Kikwete hataki kuyaweka wazi.

Kwa hakika kama Kikwete anaamini katika mazungumzo tunamwomba basi atafute muafaka na Kagame kwa njia ya mazungumzo badala ya kuendelea kurushiana maneno kupitia kwenye mikutano na hotuba. Maana naamini baada ya haya, Kagame naye atajibu! What will be next. Watanzania hatutaki vita sasa hivi. Muyamalize kama mlivyoyaanzisha.

Wewe nia yako ni kumfutia Kagame unduli wake kwa eneo hili, kwani ufahamu kuwa Kagame ndiye Zimwi??!. Naona unajizunguuusha kama feni ya kichina. Nikuulize wewe kiazi, kati ya Kikwete na huyo bwana ako ni nani aliemtukana mwingine? na kumzalilisha kama vile Kikwete ni Rais wa TFF. Labda kama akikutanishwa lakini sio ajikutanishe mwenyewe!!. Kuna picha mnataka kucheza hapa.
 
Sasa wewe Kiazi ushauri wako ni nini? Tunafanyaje kumaliza hizi tofauti zilizopo katika ya Kikwete na Kagame? Maana ni dhahiri kwamba Kagame hawezi kumuomba radhi Kikwete, je wewe unasemaje juu ya hilo?
 
Huyo Kagame ni mnafik, kwani Kikwete aliposema aongee na hao jamaa Kagame si alikuwepo hapo hapo na hakujibu chochote, kuondoka hapo ndio anajidai kusema alipofika kwao. Kama mwanamme kweli si angeongea mbele ya wanaume wenzake.

ukimya wa Kagame baada ya hotuba ya JK ni fedheha kwa Taifa
 
hv kwa mfano kama wakisema wazichape kavukavu kati ya Jk na Kagame nani atasanda?
 
Mkuu una busara ya hali ya juu.Ni watu wachache hapa JF.wenye upeo kama huo.Mungu akubariki sana sana.Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.Kwa kweli mimi nimesikitika sana kuona hawa majirani zetu ni kama yatima,walipatwa na matatizo kwenye Genocide .Badala ya sisi kuwaweka sawa sisi tunawachukia bila ya kujua ugomvi wao ndani ya nchi.Kwa kweli kikwete alitakiwa afanye kama Mandera au Mwalimu nyerere alivyokua anatatua ugomvi pale Burundi.Hawa wenzetu bado wana mawenge ya kuuana.Ungejua Kagame analishawaambia hao waasi warudi kujenga nchi.kuna wengine wamerudi ,lakini wengi bado wanaendesha majeshi huko congo.Kama mkuu ulivyosema mkuu wetu hana simu ya Kagame?.Kumpigia haina maana umejishusha hapana.huu ugomvi unaonekana ulianza siku za nyuma.Tunawafukuza ndugu zetu majirani tunawapokea wachina,wairan,wahindi ,wanigeria n.k.Kibaya tunajenga chuki sasa hivi kati ya hizi nchi.Impact yake sio leo watoto wetu watakuwa katika wakati mgumu sana.Tuwe na akili na mawazo ya kutazama mbele kwa ajili ya vijazi vyetu na sio hawa marais wawili wanaogombana sasa hivi.Mungu utuepushe na vita .Amen
 
ukimya wa Kagame baada ya hotuba ya JK ni fedheha kwa Taifa
du sasa ulitaka Kagame ajibu nini ilihali ameambiwa ukweli na ukweli siku zote mchungu. Isitoshe hii sio Kombolela au mchezo wa pwagu na pwaguzi. Hivi na mwanzo ulisema hivyohivyo ukimya wa kikwete baada ya matusi na kejeli kutoka kwa kagame na mshikiwabo ni fedheha kwa Rwanda au uliona ni sawa tu. JISACHI.

nyinyi ndio wale wa ukinipiga umenionea ukiniacha umeniogopa! Hah
 
Inashangaza sana, na inasikitisha sana kwamba Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete, anayeamini katika mazungumzo zaidi kuliko nguvu, ameingia kwenye mkumbo uleule wa kufanya yaleyale ambayo amemshauri mwenzake Kagame aachane nayo.

Hivi kulikuwa na mantiki gani kwa Kikwete kuutangazia umma tofauti zake na Kagame ilihali anaamini katika kumaliza migogoro kwa mazungumzo? Hivi Kikwete haijui namba ya simu ya Kagame? Kwanini hajampigia simu Kagame ili wayamalize, kabla ya kutuhutubia sisi? Au kama anaona hataweza kuongea na Kagame moja kwa moja, ina maana haijui namba ya Mseveni au ya Uhuru? Ameshindwa nini kuwaomba hawa majirani wamuitie Kagame ili wapatanishwe?

Japo amejibu vema katika hotuba yake lakini maneno yake mbele ya mtusi yule yanaweza kuongeza chuki badala ya kumaliza hizo tofauti. Baada ya kutoa hotuba ile, Kikwete anadhani atakuwa amesaidiaje kumaliza tofauti zake na Kagame? Je wanaweza sasa kukaa chini na kuyamaliza kwa vile tu amesema anasikitishwa na kauli za Kagame?

Dalili zinaonyesha kwamba Kikwete ameanza kutengwa na marais wengine wa Africa mashariki. Ni dhahiri Rais wetu ni tatizo, inawezekana anaiponza nchi. Haiwezekani kwamba ushauri tu dhidi ya Kagame ndiyo uliosababisha haya yote. Lazima kuna mengine nyuma ya pazia, ambayo Kikwete hataki kuyaweka wazi.

Kwa hakika kama Kikwete anaamini katika mazungumzo tunamwomba basi atafute muafaka na Kagame kwa njia ya mazungumzo badala ya kuendelea kurushiana maneno kupitia kwenye mikutano na hotuba. Maana naamini baada ya haya, Kagame naye atajibu! What will be next. Watanzania hatutaki vita sasa hivi. Muyamalize kama mlivyoyaanzisha.
Mkuu Lukolo,husika na mstari wa mwisho wa maelezo yako,maamuzi ya vita hufanywa na mamlaka za juu kabisa katika nchi sasa je mwananchi wa kawaida vita itapotimuka unafanyaje???unakimbia au unashika spika na kusema mimi sipendiiiiiiiiii!!!!hilo ni moja lakini la pili kwa nini umlenge JK atafute suluhu na PK kama kwa hili jambo la kupewa ushauri reaction imekuwa hiyo unadhani JK ana hamu hata ya kunyanyua simu???hebu tuwe wakweli hata ungekuwa wewe Lukolo ungeweza kuwa na moyo huwo???nilishasema tena hapa PK alikuwa na mlundiko wa chuki moyoni dhidi ya JK akisubiri tu aingie kwenye kumi na nane zake akione na kweli amejifunua alivyo.ni kweli katika EAC wote tunategemeana japo kwa tofauti ya asilimia,Rwanda inaihitaji zaidi TZ kuliko sisi tunavyowahitaji wao,na ndio maana jana waziri wao wa mambo ya nje alisema kwa lugha ya upole kabla ya kuwatimua wananchi wa Rwanda yaani wahamiaji haramu TZ ingefanya mazungumzo Rwanda wakati ni siku chache zilizopita anasema JK ni symphasizer wa FDLR.
 
Nakubaliana na wewe kwamba maamuzi ya vita siku zote hufanywa na mamlaka za juu. Na pengine wananchi hatuna namana ya kupinga hilo. Lakini tuna nafasi ya kusema na uongozi wetu ili upunguze huo uwezekano wa nchi kuingia vitani. Bado hali yetu ya kiuchumi ni ngumu sana, hatustahili hata kuiota hiyo vita. kama tutaruhusu hizi chokochoko za maneno ziendelee tutaishia kupigana. Ndiyo ilivyokuwa kati ya Nyerere na Idd Amini, naona sasa inataka kutokea hivyohivyo na Rwanda. Wakati sisi tupo busy kupigana na kila jirani yetu wenzetu wa Kenya wanazidi kujenga uchumi imara. Kabla ya Vita na Idd Amini Tanzania ilikuwa ndiyo nchi imara kiuchumi AFrica Mashariki, lakini baada ya ile Vita tulishuka ghafla na kuanza kujishindwa kabisa. Tunataka tuwe wa mwisho kiuchumi katika Africa mashariki? Hatutaki vita sisi.

Ninaamini ningekuwa mimi, ningempigia simu Kagame kumuuliza kwamba nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba ananisema vibaya. kwani ushauri wangu ulikuwa na ubaya gani? Kama hakuupenda ushauri wangu basi namwomba radhi na ninaomba yaishe. Kwani JK angesema hivyo ingekuwaje? Si mazungumzo ya kwenye simu tu?K

ama Kagame angemjibu hovyo, bado JK angekuwa na nafasi ya kuwasiliana na kiongozi mwingine wa Africa kumtaka azungumze na Kagame na kumweleza nia yake ambayo ilikuwa imelenga kumaliza mgogoro na kwamba yeye JK hakujua kama wazo lake hilo lingemuumiza Kagame. Hivi ukisema hivyo unakuwa umeshuka thamani kiasi gani? Kama yeye JK anaamini katika mazungumzo na anamtaka Kagame ashuke na kuzungumza na waasi wake, ni kwa vipi yeye JK asiwe tayari kuzungumza na Kagame ambaye hawajawahi kuwa na ugomvi naye?

Kwahakika mimi bado naona JK ana nafasi ya kumuomba mwenzake kagame ili wayamalize kwa amani badala ya hii hali inayoendelea sasa ambayo inatishia usalama wa nchi hizi mbili. Tayari tuna uadui na Malawi, hatuhitaji kuwa na uadui na Rwanda tena. Hatujiulizi ni kwanini sisi tu ndiyo tunakuwa na maadui kila upande?
 
Kikwete kumwomba msamaha Kagame ni sawa na Kikwete kumwomba msamaha Diwani.
 
Kikwete kumwomba msamaha Kagame ni sawa na Kikwete kumwomba msamaha Diwani.
Kwani diwani ndiyo haombwi msamaha? Hata mwenyekiti wa kijiji anastahili kuombwa msamaha kama amekosewa. huo ndiyo ubinadamu. Mbona mimi huwa namwomba msamaha mwanangu wa miaka mitatu?
 
my president will never bow down before Kagame...
Inashangaza sana, na inasikitisha sana kwamba Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete, anayeamini katika mazungumzo zaidi kuliko nguvu, ameingia kwenye mkumbo uleule wa kufanya yaleyale ambayo amemshauri mwenzake Kagame aachane nayo. Hivi kulikuwa na mantiki gani kwa Kikwete kuutangazia umma tofauti zake na Kagame ilihali anaamini katika kumaliza migogoro kwa mazungumzo? Hivi Kikwete haijui namba ya simu ya Kagame? Kwanini hajampigia simu Kagame ili wayamalize, kabla ya kutuhutubia sisi? Au kama anaona hataweza kuongea na Kagame moja kwa moja, ina maana haijui namba ya Mseveni au ya Uhuru? Ameshindwa nini kuwaomba hawa majirani wamuitie Kagame ili wapatanishwe? Japo amejibu vema katika hotuba yake lakini maneno yake mbele ya mtusi yule yanaweza kuongeza chuki badala ya kumaliza hizo tofauti. Baada ya kutoa hotuba ile, Kikwete anadhani atakuwa amesaidiaje kumaliza tofauti zake na Kagame? Je wanaweza sasa kukaa chini na kuyamaliza kwa vile tu amesema anasikitishwa na kauli za Kagame? Dalili zinaonyesha kwamba Kikwete ameanza kutengwa na marais wengine wa Africa mashariki. Ni dhahiri Rais wetu ni tatizo, inawezekana anaiponza nchi. Haiwezekani kwamba ushauri tu dhidi ya Kagame ndiyo uliosababisha haya yote. Lazima kuna mengine nyuma ya pazia, ambayo Kikwete hataki kuyaweka wazi. Kwa hakika kama Kikwete anaamini katika mazungumzo tunamwomba basi atafute muafaka na Kagame kwa njia ya mazungumzo badala ya kuendelea kurushiana maneno kupitia kwenye mikutano na hotuba. Maana naamini baada ya haya, Kagame naye atajibu! What will be next. Watanzania hatutaki vita sasa hivi. Muyamalize kama mlivyoyaanzisha.
 
Dawa ya moto ni moto; watu kama hao ukiwapa kidole watakuvuta mkono mzima.

Kagame hajui diplomacy, kwa hiyo ukisema utumie diplomacy kwake utakuwa unatwanga maji kwenye kinu; iwapo diplomacy ingekuwa inafanya kazi kwa Kagame asingetamka maneno aliyosema dhidi ya Kikwete, na yeye angetafuta njia za kidplomasia kumwonyesha Kikwete kutoridhishwa na ushauri uliotolewa na huyo Kikwete.
 
.... Kama mwanamme kweli si angeongea mbele ya wanaume wenzake.

Ili neno la kuudhi...hapa uliaribu mfungo...lazima ulipe mfugo huu.

Nikirudi kwenye mada

FF...uanaume wa kweli...hauhalalishi kuongea bila kutafakari...ni busara tu ya Kagame iliyomuongoza asiseme chochote pale. Busara hiyo imuhakikishia kuwa kwa kuwa mtoa hoja "hatabiriki" basi akisema chochote wanaweza kukunjana kwenye nchi ya kigeni...na kuleta aibu ya mwaka ugaibuni (kumbuka wote ni maaskari).
 
Dawa ya moto ni moto; watu kama hao ukiwapa kidole watakuvuta mkono mzima.

Kagame hajui diplomacy, kwa hiyo ukisema utumie diplomacy kwake utakuwa unatwanga maji kwenye kinu; iwapo diplomacy ingekuwa inafanya kazi kwa Kagame asingetamka maneno aliyosema dhidi ya Kikwete, na yeye angetafuta njia za kidplomasia kumwonyesha Kikwete kutoridhishwa na ushauri uliotolewa na huyo Kikwete.
Kagame pia ameamua kutumia hiyo approach ya dawa ya moto ni moto, ili kupambana na waasi wa FDRL kule Congo, lakini Kikwete, amemchalenge kwamba dawa ya moto ni kumwagia maji. Kama Kikwete anaamini katika kupooza moto kwa kumwagia maji, basi aonyeshe kwa vitendo kauli yake kwa kumuomba radhi Kagame ili asiingize nchi vitani.
 
huyu kama ni mtz ni -------- wa kwanza. Kikwete doesnt need to talk to that useless kagame. Ni ushauri ulitolewa. its either you take it or you leave it. wewe mtu ni mjinga tena msaliti wa kwanza. huna akili kabisa weeewe.
 
kapigane wewe peke yako na husituushishe wangoni wote sawa.Sisi tunataka kujenga uchumi.Hatutaki vita.kama kuna bajeti ya vita hivi sasa naomba tuipeleke kwenye shule zetu na kwenye zahanati huko vijijini.
 
Raisi wetu sio tatizo ila hao wengine kwa vile walitaka kumtumia kuwasaliti watanzania kwa kuwaachia rasilimali zao. Mimi siku zote nitamheshimu sana J. Kikwete kwa uzalendo wake.
Huna Jipya... JK nijanga ,elewahilo..
Rais hana dira..
Rais hana tamko..
Rais hana msimamo..
Rais hajui mamlaka yake..
Rais hajui nini anapaswa kufanya kama kiongozi mkuu kwa Taifa lake..
Rais yupo yupo tuuuu... Ana cheeekaaa tuuuu...
Then mnataka akae meza moja na Marais wanaojitambua?
Wao wanawaza maendeleo ya nchi zao,
Wao wanawaza ni jinc gani watatekeleza ahadi zao kwa wapiga kura wao,
Rais wenu anachekaa tuuu....
J= Janga
K= Kuu.
 
Ili neno la kuudhi...hapa uliaribu mfungo...lazima ulipe mfugo huu.

Nikirudi kwenye mada

FF...uanaume wa kweli...hauhalalishi kuongea bila kutafakari...ni busara tu ya Kagame iliyomuongoza asiseme chochote pale. Busara hiyo imuhakikishia kuwa kwa kuwa mtoa hoja "hatabiriki" basi akisema chochote wanaweza kukunjana kwenye nchi ya kigeni...na kuleta aibu ya mwaka ugaibuni (kumbuka wote ni maaskari).

Kagame ni was Mpiganaji
JK was mbeba Gwanda...
 
Back
Top Bottom