Kikwete, zungumza na Kagame!!

Mkuu Lizaboni isije ikawa kinyume chake, maana JK naye ni fedhuli kuwanyazia wauza unga, vijana wa afrika wanaharibika.
 
Kagame ndio azungumze na kikwete kwani mtu aliyekuwa akibwabwaja sana na kuitisha vikao baada ya vikao na kutoa vitisho ni kagame while dr jk alikuwa busy na hamsini zake
 

Kwani uliambiwa kuna ugomvi baina ya Kikwete na Kagame? Kikwete alipoyasema hayo si alisema na Kagame yupo? Sasa ni Kagame amma aongee na wahutu amma aendelee kutukana anyukwe na dunia nzima.
 
Huyo Kagame ni mnafik, kwani Kikwete aliposema aongee na hao jamaa Kagame si alikuwepo hapo hapo na hakujibu chochote, kuondoka hapo ndio anajidai kusema alipofika kwao. Kama mwanamme kweli si angeongea mbele ya wanaume wenzake.

Ametoa sababu nne za kwanini hakuongea neno lolote.

 
Last edited by a moderator:
Hivi raia wa kawaida utajuaje kama JK hajampigia simu PK?
Kama angekuwa amempigia na hakujibiwa au alijibiwa kwa jeuri, angeliweka hayo kwenye hotuba yake.
 
Kwa vile wewe unamtetea dr slaa ambaye ndiye fisadi namba moja ndani ya chadema na mzinzi mkubwa, basi na wewe ndo uko hivyo? Wewe ndo unatumika vibaya na wala unachoandika hakina mwelekeo. Hizo ndo ishara kuwa kijana unatumika


Lizaboni,
alizini na wewe nini mbona unaujua sana uzinzi wake?

LL
 
Kwahakika hakuna popote ambapo namuona Kikwete kuwa na tatizo. Ninachokisema hapa ni kwamba badala ya kuja kwenye halaiki na kutuhutubia jinsi rafiki yake huyu wa siku nyingi alivyogeuka na kumchukia, alikuwa ana nafasi ya kuongea na akina Museveni au Uhuru ambao tayari wanaonyesha kila dalili za kuegemea kwa Kagame kuliko kwa Kikwete. Angeongea nao awaombe wamuulizie Kagame ni nini kinachosababisha atoe maneno makalimakali kama hayo? Na ikiwezekana angeomba upatanisho. Kwani tatizo liko wapi kama angefanya hivyo? Maana baada ya hotuba ya Kikwete, hatujui, Kagame atajibu nini na mwisho wake utakuwaje? Badala ya kuendeleza malumbano ya kwenye hotuba, kwanini wasikae chini waongee?
 

Pia ni vyema akakutana na Babu Seya.
 
Kwa hiyo unataka ufanyeje na Kagame? Watanzania hatutaki vita sasahivi. Vita ya Uganda tu imetusababishia umaskini mkubwa ambao unaendelea kuwaumiza watanzania hadi leo, bado mnatuletea kejeli za vita tena, huku mateso yatokanayo na vita ilivyopiganwa miaka 30 iliyopita bado hayajaisha?
 
Mkuu, kuna wakati nilishawahi kusema kuwa hawa bavicha si watu wa kawaida bali ni misukule ya dr slaa na mbowe. Watu gani wanashindwa kuwa na mawazo huru na msimamo thabiti?

jana nilisema hawa bavicha kama wametoka kikaoni na dk slaa, wanaongea vitu vya ajabu toka silaha atoe ubishi wake ule
 
Vijana wa Bavicha tangu Slaa amuunge mkono Kagame mmeamua na nyinyi Kujiunga naye!

Siasa za namna hii sio healthy kwa ustawi wa Taifa...

Mkuu, kuna wakati nilishawahi kusema kuwa hawa bavicha si watu wa kawaida bali ni misukule ya dr slaa na mbowe. Watu gani wanashindwa kuwa na mawazo huru na msimamo thabiti?
Haya hayatusaidii. We are all Tanzanians and we love our country.

Kama wazo la Kikwete kukutana na Kagame ili wayazungumze na kuyamaliza, kwenu linaonekana ni la kibavicha, lipi basi ni wazo lenu? Tuingie vitani na Rwanda? Muungwana hashambulii mtu bali anashambulia hoja. Hoja iliyotolewa ni kumuomba Kikwete azungumze na Kagame ili kumaliza hizi tofauti zilizopo. Tena imependekezwa kwamba awatumie Uhuru na Museveni ili wawapatanishe.

Tunajua Kagame ana jeuri lakini kwa sasa hatuna namna hatuwezi kuintertain malumbano yasiyo na tija. Naamini Kikwete alitoa maoni yake binafsi wala hayakuwa maoni ya Tanzania kwamba Kagame aongee na mahasimu wake. Sasa hoja binafsi za watu binafsi zisiipeleke nchi yetu vitani. Waombane radhi wayamalize. Kama nyie mna hoja tofauti na hii, basi ileteni na si kuandika kwa kejeli bila ya kujenga hoja.
 
Nonesense.LUKOLO.
Yaani Anthony na Clinton wawe envoy ya KIKWETE kwa Kagame?HAYA NDO MATATIZO YA HEROINE NA COCAINE.
 
Nonesense.LUKOLO.
Yaani Anthony na Clinton wawe envoy ya KIKWETE kwa Kagame?HAYA NDO MATATIZO YA HEROINE NA COCAINE.


Mkuu ukiamini katika meza ya maapatano si uoneshe mfano, yaani kikwete aoneshe kwa vitendo sio hotuba.

Kikwete aoneshe mfano kwa:-

1. Kuongea na waalimu mezani sio kutishia kuwapiga

2. kuongea na madakitari mezani sio kuwafukuza kazi na kuwapiga

3. kuongea na kukubaliana na wapinzani hususani chadema mwanza na Arusha

4. Aongee na kagame mezani sio kutuhutubia kwa ushairi na mipasho

Akifanya hayo labda naweza kumuelewa vinginevo nitaendelea kupingana nae, nitaamini afanyao kikwete ni usanii na

propaganda baada ya sera ya maisha bora kwa kira mtanzania kumshinda sasa anatafuta huruma ya jukwaa la

kimataifa kwa unafiki maana yeye hafanyi hivo ila wenzie wafanye!!!???
 
MSIMAMO WANGU TOKA MAPEMA.
siungi mkono vita kwa upuuzi wa maneno maneno ya ugomvi wa maraisi.
KAMA WAMEGOMBANA KWA SABABU ZAO WAISHIE HUKO HUKO wasiingize nchi katika vita vya kijinga.
TUNA MAMBO MENGI NA MAGUMU NA NI YA MSINGI SANA KAMA TAIFA YANAHITAJI KUFANYWA.
Najua raisi anapaswa kulindwa ndio mana anawalinzi,na ninajua ana maadui na kuna watu wanataman kumfanyia lolote baya LAKINI WALINZI WAPO kwa ajili yoyote.
NI WAJINGA PEKEE WANAWEZA KUIINGIZA NCHI VITANI KWA TOFAUTI YA MANENO.
Vita zote hutokea baada ya usalama wa nchi kutishiwa,Hugo Chaves alimuita Bush shetani,King Jon Un kagombana na S.KOREA na usa,Mugabe na UK AND USA nk lakini hakuna aliyeenda vitani.
KAGERA MPAKA tulipigwa ndio ikatosha kuchukua hatua na si maneno maneno ya nyerere na idi amin.

WAONGEE WASIONGEE LAKINI HAKUNA KWENDA VITANI KWA SABABU ZA MANENO NINAZOZIITA ZA KIPUUZI.
lakini kwa mfano akitufyatulia hata kombola moja basi sawa mana ni uchokozi uliopitiliza
 
LUKOLO.
hujanielewa,nilikuwa najibu comment yako kuwa Anthony na Clinton ni envoy kwa kagame.HII NI NDOTO YA MCHANA.

MIMI BINAFSI.
siungi mkono tamko la hadharani la Raisi wangu.
NINGEKUWA MIMI.
ningetoa tamko la chini kwa chini mana kagame hakutoa hadharani na leo anaweza kukanusha kuwa hakuwahi kumtukana kikwete na kusiwe na ushahidi.
LILE TAMKO LA KAGERA NALIUNGA MKONO MANA LILIKUWA INDIRECT ila wenye akili tulilielewa.
ALICHOFANYA SASA NI KUWEKA PETROL KWENYE MOTO.

Binafsi siwezi kumlazimisha JK azungumze na kagame.

ILA HAKUPASWA KUONGEA HADHARANI.
Japo naunga mkono hoja ya kuzungumza nae.
 
Mshinga, kwenye post yangu namba 25 nimeweka ushahidi wa video ya Kagame akitangaza hadharani kwamba Kikwete ni ignorance, alisema mambo ya kipuuzi etc. So ni wazi kwamba Kagame alisema hadharani.

Nakubaliana na wewe kuhusu suala la vita. Kwahakika hatupaswi hata kuota habari za kwenda kupigana na yeyote. Maana tutapoteza watu wetu, na mali zetu kwa sababu zisizo na maana, ndiyo maana nasema Kikwete na Kagame wayamalize bila kuiathiri nchi. Badala ya kuhutubia watu wao juu ya tofauti zao, wakutane wenyewe waongee wamalizane.

Kama ambavyo adolay amesema; kama wewe ni muumini wa mazungumzo, ni kwa vipi wewe mwenyewe usionyeshe mfano wa kumaliza tofauti zenu kwa mazungumzo? Tayari Kagame ameshatishia kumpiga Kikwete, definitely Kagame amejiandaa kwa vita. Sasa tuingie vitani kwa kuwa tu eti mtu binafsi alitoa hoja binafsi isiyokuwa msimamo wa nchi? Kwanini yeye aliyeitoa hiyo hoja asiongee na mwenzake ili wamalizane bila kuiathiri nchi?
 
kwa nini isiwe Kagme aongee na Kikwete ila kKikwete aongee na Kagame hii haiwezekani Kagame kama ni mwanamme ushauri aliopewa angejibu palepale asingesubiri akacheze zeze nyumbani kwake tena kwa kutoa maneno ya kejeli na matusi pamoja na kutumia vyombo mbalimbali vya habari kumkashifu raisi wetu. Hicho alichofanya Kagame kinadhihirisha kuwa ni mwoga na mnafiki anayependa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Huku akiitumia Genocide aliyoianzisha mwenyewe kama chambo.

Kagame ndio anapaswa aongee na Kikwete maana yeye ndiye kaanzisha ugonvi wa mawe kwenye nyumba ya vioo.
 
mimi nashukuru Rais wetu kulihutubia taifa maana ile sintofahamu ya nini ni nini angalau tumeijua. Kwani wewe hata mtanzania aliye kijijini angalau sasa anajua kuna nini kati ya Rwanda na Tanzania. Yeye Kagame hujui pia kuwa anaendesha propaganda kuanzia midugudu kwa ajili ya kuihujumu Tanzania. Kweli hawa wana lao Jambo ingekuwa vizuri waliseme.

Watanzania tusiwe waoga ni wakati wa kuitetea Tanzania hata kama ni kugharimu maisha ili yanayotokea Kongo yasije kutokea Tanzania.
 


Mimi hilo la nchi jirani kututenga ndio hasa nalihitaji. Tumechoka huu ushirikiano wa kisanii wa africa mashariki. Tunaweza kuendelea wenyewe kama nchi bila kutegemea ushirikiano huu ambao hatujui hasa nia za washirika wengine kwa nchi ya Tanzania. Kaka kweli kuna ushirikiano wa dhati kwa nini maraisi wa nchi hizo tatu wakutane bila kumshirikisha rais wa Tanzania ambaye nchi yake ndio makao makuu ya Afrika Mashariki na ndiyo yenye eneo kubwa kuliko nchi hizo zote kwa pamoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…