Kikwete, zungumza na Kagame!!

Ni kweli hakusema moja kwa moja ni nini kifanyike lakini maana yake ilikuwa very clear. Na akina Kagame na Mseveni walimwelewa vizuri anachomaanisha.
 
Well, utawasema akina Mseveni kwamba waliingia kwa njia ya mtutu, but Kagame hakuingia kwa njia ya mtutu, wala Uhuru hakuingia kwa njia ambazo ni tofauti na zile alizoingilia Kikwete. Tusijidanganye kwamba Tanzania ni more democratic kuliko Kenya. Uchaguzi wa mwaka huu kule Kenya ulikuwa more democratic kuliko chaguzi zetu nyingi za hapa bongo. Kikwete hana ubora wowote unaowazidi wengine.
Unauliza mengine ni yapi; basi ninapenda kukueleza kwamba those boys in the east African community think that Kikwete is a puppet of the big boys from the western countries. Wanaamini kwamba Kikwete anajipendekeza huko ili apate misaada zaidi huku akiwachongea wenzake ili wachukiwe. Na hata wazo hilo alilolitoa Kikwete kwa Kagame mbele ya Ban Ki Mon, lilionekana ni mwendelezo wa Kikwete kujipendekeza kwa wakubwa.
 

dah! sasa sijui hata nianzie wapi, so how did kagame come into power in Rwanda? Kuhusu hayo mengine ni kweli, demokrasia chini ya kikwete sio nzuri. lakini napinga kuwa anawachongea wenzie ili wachukiwe, kwa lipi hasa? kwanza nani kasema kupata misaada kwa nchi moja ni at the expense ya nyingine?
 
Kaka huyo jamaa anaemtetea kagame ni mnyarwanda atakuumiza kichwa,hajui lolote na zumbukuku!! Hakumbuki mauaji ya kimbari yalitokana na nn na kwann wanyarwanda wenzie hawataki kurudi kwao na usikute hata yeye yupo hapa na ole wake tukishamkamata atatujua sisi watanzania tukoje,kagame achokoze moto halafu aone majibu yetu.
 
Sasa unachoshangaa ni nini? Kama hujui historia si unanyamaza tu? Kwani wewe hujui kwamba baada ya vita Rais wa Rwanda alikuwa ni Bizimungu hadi kufikia mwaka 2000? Na hujui kwamba Kagame alipokea urais kuanzia mwaka 2000 kutoka kwa Bizimungu?
Well, tufanye kwamba Kikwete hana tatizo, sasa tujiulize ni nini kinachoifanya Tanzania inyanyapaliwe hivyo kwenye jumuia ya Afrika mashariki?
 
Style ya uandishi wako tu inaweza kusema umri wako na kiwango chako cha Elimu. Umepata nafasi ya kwenda chuo gani? Au unakwenda kusoma ualimu grade A? Jenga hoja, siyo unakuja na maneno ya kishabiki hapa. Kwa uelewa wako mauaji ya Kimbari yalitokana na nini? Humu JF kuna kila aina ya watu kuna wengine humu wanapenda waonekane wanajua kila kitu hata kama hawajui.
 

Nani aliyemkataza Kagame kukaa meza moja na Kikwete? Hivi unajuwa kuwa Kikwete kisha kuwa diplomat namba moja Tanzania kwa miaka 10 mfululizo au hujui hilo?

Hivi hujamsikia Kikwete akisema kuwa huo aliotoa ni ushauri tu na si lazima kufatwa, sasa jiuize kwanini Kagame apande juu ya majukwaa na kusema na kujidai kutisha watu hovyo? Jibu; Kagame ni "mfa maji...
 
nashangaa unavyosahau kuwa kagame alishambulia serikali halali ya rwanda toka 1990 hadi 1994 kwenye 'genocide'. Na baada ya waasi/terrorists wake wa RPF kuchukua madaraka walimweka Bizimungu kuwa figurehead president na yeye akiwa real president masquerading as vice president, ili kuleta picha kuwa wahutu nao wamo kwenye uongozi.
nashangaa unavyosema kuwa 'alipokea' urais kwa Bizimungu badala ya kuupora kupitia frustations alizompa kwa kumzushia tuhuma za uongo zilizopelekea Bizimungu kupewa miaka 15 for god knows what..
anyway what was Kagame's former occupation right before the 'genocide'...At best, a REBEL! sasa unavyosema huoni Mtutu hapo kwa nini nisishangae?
Tanzania inanyanyapaliwa kwa misimamo yake ya haki!
 

hii hali inatisha aisee inabidi kuomba mungu aepushe hili balaaaa....
mi sijui nini hasa root ya mgogoro....naona tu vitisho na maneno mara hivi mara vile...am confused
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…