Kila anayefanya vibaya serikalini uhamishwa na kulipwa gharama za Uhamisho zisizopungua milioni kumi kwa mtumishi mwandamizi na 25M kwa wakuu wa Idara

Kila anayefanya vibaya serikalini uhamishwa na kulipwa gharama za Uhamisho zisizopungua milioni kumi kwa mtumishi mwandamizi na 25M kwa wakuu wa Idara

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Only in Tanzania ndipo kufanya kazi kituoni muda mrefu ni kigezo cha kushuka ufanisi. Tanzania Uhamisho wa watendaji ni maamuzi ya kila mtu. Hakuna sera inayoongoza taratibu za uhamisho.

Leo kwa kauli za wakuu wetu mganga mbobezi anaweza kuhamishwa kituo kisa amekaa muda mrefu; wakuu wa Idara wanaweza kuhamishwa vituo kwa sababu ya muda.

Let us calculate amount ya fedha inayotumika kuhamisha watumishi ni kiasi gani? Ukisoma ripoti ya CAG, utagundua baada ya madeni ya wakandarasi deni kubwa linalofuata ni uhamisho.

Kwa mahesabu madogo, mkuu wa Idara akihamishiwa analipwa si chini ya milioni ishirini na tano kama gaharama za uhamisho. Katika mazingira ya uchumi mbovu duniani uhamisho si kipaumbele hasa ikizingatiwa mahitaji ya fedha katika huduma ni makubwa.

Mhe. Rais alipokabidhiwa nchi alitoa maelekezo kwa viongozi wote kwamba hakuna uhamisho bila malipo. Kwa msingi huo wakuu wa Idara wanapotangaziwa uhamisho kwao ni neema kwa sababu wanapewa 25M cash lakini pia kwa wananchi ni hasara kwa sababu kubadili vituo vya kazi siyo kubadili mindset. Ni kuhamisha tatizo kwa kulilipia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Niombe sasa wakuu wa mikoa na wilaya wafanye kama alivyoelekeza mkuu wa mkoa wa Arusha, wizara zifanye the same na kila Idara na taasisi zifanye kuboresha utoaji huduma.

Wizara ya mipango na wizara ya utumishi msipowadhibiti wateule fedha za maendeleo zitaendelea kutumika kuhamisha matatizo kila baada ya miaka mitano. Kama kiongozi anaona mkuu wa Idara hana tija anachotakiwa kufanya ni kupendekeza avuliwe madaraka siyo kumlipa milioni 25 za uhamisho. Tukiendelea kuwalipa wanaharibu fedha za uhamisho tunawavunja moyo wanaofanya vyema kwa sababu wao awatalipwa
 
Umeongea kitu muhimu sana wahusika wanatakiwa walifanyie kazi ni uwazi usiopingika inakuwaje mkuu wa idara kaharibu sehemu moja nahamishiwa sehemu nyingine swali la kujiuliza huko anakohamishiwa wananchi wanahitaji huduma mbovu kutoka kwa huyo mtumishi aliyehamishiwa eneo hilo kutoka huko aliko haribu jibu ni hapana,, tiba ya hili jambo akiharibu ashushwe cheo naamini kuna watumishi chini yake au kutoka sehemu nyingine wanafanya kazi vizuri apewe nafasi hiyo.
 
Back
Top Bottom