Kila atakayeifunga Simba kusajiliwa?

Kila atakayeifunga Simba kusajiliwa?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sasa hii imekuwa tabia au hulka, Tulipofungwa na UD SONGO mchezaji aliyetufunga akasajiliwa , leo tena Chikwende naye ndio kama mlivyosikia .

Bado haijafahamika kama usajili huu ni pendekezo la Kishingo au Matola, ama labda Babra , wala haijulikani kama usajili huu unakidhi vigezo vya kiufundi, bali kinachofahamika ni kwamba Chikwende amesajiliwa Simba baada ya kuidungua goli kule Harare hata kama mpira ulimgonga kwenye ugoko
 
Usajili wa mihemko kama ule wa morison,saizi wanataka kumtema wanamsingizia ugonjwa!
 
Sasa hii imekuwa tabia au hulka , Tulipofungwa na UD SONGO ya Angola mchezaji aliyetufunga akasajiliwa , leo tena Chikwende naye ndio kama mlivyosikia .

Bado haijafahamika kama usajili huu ni pendekezo la Kishingo au Matola , ama labda Babra , wala haijulikani kama usajili huu unakidhi vigezo vya kiufundi , bali kinachofahamika ni kwamba Chikwende amesajiliwa Simba baada ya kuidungua goli kule Harare hata kama mpira ulimgonga kwenye ugoko
Duuuh kwenye ugoko
 
Sasa hii imekuwa tabia au hulka , Tulipofungwa na UD SONGO ya Angola mchezaji aliyetufunga akasajiliwa , leo tena Chikwende naye ndio kama mlivyosikia .
Mkuu kwani unateseka nini, ina maana huioni kazi ya Luis Miquissone? Huioni kazi ya Bocco? Mugalu, Chama na Larry Bwalya waliifunga Simba lini? Kwenye utafiti huwa hatutoi conclusion kwa kuangalia sample chache namna hiyo, ndiyo maana huwa tunasisitiza watu waongeze maarifa
 
Morrison, Luis na sasa Chikwende
Mkuu kwani unateseka nini, ina maana huioni kazi ya Luis Miquissone? Huioni kazi ya Bocco? Mugalu, Chama na Larry Bwalya waliifunga Simba lini? Kwenye utafiti huwa hatutoi conclusion kwa kuangalia sample chache namna hiyo, ndiyo maana huwa tunasisitiza watu waongeze maarifa
 
Halafu wanasajili mtu asiye na vigezo vya kucheza champions leage, sijui wa nini
 
Hebu weka ushahidi wa kikanuni kusapoti hii hoja yako tafadhali.

Ninachojua kanuni za CAF kwa mashindano ya champions league ya msimu huu zinaruhusu mchezaji aliyecheza timu A katika mashindano hayo kuhamia timu B na kuichezea.

Ukiweka kipengele kinachokataza hili, ambacho uongozi wa Simba haukijui na hata wakamsajili ''mdaawa'' Chikwende, utakua umenisaidia sana.
 
Sasa hii imekuwa tabia au hulka , Tulipofungwa na UD SONGO ya Angola mchezaji aliyetufunga akasajiliwa , leo tena Chikwende naye ndio kama mlivyosikia .

Bado haijafahamika kama usajili huu ni pendekezo la Kishingo au Matola , ama labda Babra , wala haijulikani kama usajili huu unakidhi vigezo vya kiufundi , bali kinachofahamika ni kwamba Chikwende amesajiliwa Simba baada ya kuidungua goli kule Harare hata kama mpira ulimgonga kwenye ugoko

Hivi ukiwa unatafuta mchezaji wa nafasi ya kufunga (mshambuliaji au kiungo mshambuliaji), ni vigezo vipi vinatumika nje na uwezo wa mchezaji huyo kufunga ?

Kama tunaangalia uwezo wake wa kufunga, unataka awe amemfunga nani ndio ujue kwamba mtu huyu ni mfungaji ?
Je, akikufunga wewe anapoteza sifa za yeye kuwa ni mfungaji ?

Mimi nadhani ni jambo jema sana kuanza na yule aliyekufunga wewe, ukaangalia rekodi zake za kuwafunga wengine kisha ukamwajiri awafunge wengine akiwa upande wako.
 
Sioni ubaya hata kidogo kwa hilo kama mchezaji atakuwa mzuri, mfano konde boy.
 
Sasa hii imekuwa tabia au hulka , Tulipofungwa na UD SONGO ya Angola mchezaji aliyetufunga akasajiliwa , leo tena Chikwende naye ndio kama mlivyosikia .

Bado haijafahamika kama usajili huu ni pendekezo la Kishingo au Matola , ama labda Babra , wala haijulikani kama usajili huu unakidhi vigezo vya kiufundi , bali kinachofahamika ni kwamba Chikwende amesajiliwa Simba baada ya kuidungua goli kule Harare hata kama mpira ulimgonga kwenye ugoko
Mbumbumbu fc aka utelembwe
 
Back
Top Bottom