Kila ikifika jioni socket breaker inaanza kuzima mara kwa mara

Kila ikifika jioni socket breaker inaanza kuzima mara kwa mara

Jioni kuanzia saa 11 mpaka saa2 na nusu ukiwasha circuit breaker inazima kila baada ya dakika kadhaa, ila muda mwingine wote umeme hauzimi.

Wataalamu wa haya mambo naomba msaada.
uko na wapangaji watumishi wa serikali au uko kwenye nyumba yako unaishi na familia yako tu
 
Sidhani kama RCD ambayo haitrip ndo "nzuri" kazi ya RCD ni kutrip pale panapokuwa na "leakage" ya umeme, kwa jinsi ulivyoeleza tatizo kuna kifaa kitakuwa kina matatizo, hasa tatizo kama la waya wa live kugusa body ya kifaa e.g jiko, hii ni hatari kwa mtumiaji kwa vile unaweza kupigwa na umeme pale unapogusa kifaa, unapogusa wire live umeme unapita katika mwili wako na kuingia ardhini, so huu umeme unakuwa umeleak kutoka kwenye circuit, RCD inaweza kudetect hii hali na kuzima umeme papo hapo ndani ya 30 milliseconds na kuoka maisha yako so hiki kifaa ni kwa ajili ya kulinda afya ya binadamu.

Pia vifaa vyenye waya wa earth vinalinda afya yako kwa kupeleka umeme ardhini kama kuna tatizo na kifaa, RCD itadetect hiyo leak inayoenda earth na kukata umeme.

So kuweka RCD ambayo haizimi aka haifanyi kitu inaweza ikawa in umeweka kifaa ambacho hakifanyi kazi yake.
 
Back
Top Bottom