mrdocumentor
Member
- Nov 27, 2021
- 45
- 56
Tarehe 17 March 2021 ni mwaka ambao watanzania kwa mara ya kwanza walishuhudia tukio ambalo halikuwahi kutokea kabla, Tukio la kiongozi mkuu wa nchi, raia namba moja, Amir jeshi mkuu na mwenyekiti wa chama tawala Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli alitoweka katika ulimwengu huu. Kwa mujibu wa madaktari walithibitisha kuwa mpendwa wetu alitoweka kwa matatizo ya moyo richa ya maneno mengi ambayo yaliambatana na kifo hicho maneno ambayo kwangu yalikuwa ni matokeo tu ya kuwa watanzania walimpenda sana kiongozi huyu ndio maana kwa namna fulani wengi wao hawakutaka kuamini kuwa kipenzi chao kimetoweka kwa hali ya kawaida tu.
Baada ya kifo cha Magufuli kama ilivyo kwa mujibu wa katiba yetu aliyekuwa makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan alikabidhiwa kiti cha urais na kuanza majukumu yake mara moja.
Watanzania iliwachukua mda sana kumuelewa mama kwa sababu walitegemea namna mtangulizi wake alieyepita alivyokuwa anaongoza nchi ndivyo hivyo hivyo mama atakavyoongoza jambo ambalo halikuwa hivyo, yapo mambo mengi ambayo kimtazamo yalionekana wazi kuwa tofauti na mtangulizi wake kama vile:- namna ambavyo alishughulikia janga la UVIKO 19, Kuwarudisha wajawazito shuleni baada ya kujifungua na mengine mengi ambayo yalikuwa tofauti na mtangulizi wake.
Taharuki ilitanda kwa watanzania wengi na wengine walifikia hatua ya kumlilia hayati Maguful kila siku wakiamini yeye pekee ndiye anayeweza kubadilisha vile ambavyo kwao waliona haviendi sawa, na si kwa wakati huo tu bali hadi sasa lipo kundi kubwa la watu ambao wameachwa na athari za mitazamo na misimamo ya Hayati Magufuli ambao bado hadi kesho wanaona mambo kama yanawaendea tofauti kwao.
Jambo ambalo watu wengi hawakulifahamu au hawalifahamu hadi sasa ni kwamba falsafa za uongozi kwa mtu mmoja na mwingine haziwezi kufanana ikiwa hakuna muongozo mmoja unaowaongoza watu hao. Kwa nchi yetu kwa sasa hamna dira inayomuongoza Rais apite njia gani ili kufikia kile ambacho kama nchi tunakihitaji, jambo ambalo linapelekea kila kiongozi anapokuja anakuwa na muongozo wake binafsi kulingana na kile anachokiamini na hapo ndio mwanzo wa tatizo na taharuki kwa wananchi kwa sababu wakati Mwananchi wa kawaida anategemea kiongozi anaekuja aendeleze pale alipoishia aliepita mda huo huo kiongozi husika anafikiria kuja na kitu tofauti na aliyemtangulia matokeo yake Kiongozi wa muda huo anakutana na upinzani wa aina mbili yaani wa vyama pinzani na kundi la wananchi wanaoamini katika dhana na falsafa za kiongozi aliepita.
Jambo la msingi ili kuondoa changamoto hiyo ni lazima kama nchi iwe na dira ambayo kila kiongozi atakayeingia madarakani itamuongoza kufikia malengo ya taifa letu, na jambo hili limeshazungumzwa sana hata Mheshimiwa Josephat Gwajima amewahi kulitolea hoja hili katika moja ya vikao vya bunge. Na dira ni muhimu sana kwa sababu kama tutaendelea kuongozwa bila muongozo maalum, kwanza tujiandae kukubaliana na kila jambo linaloletwa na kiongozi husika kwa wakati wake lakini pia athari nyingine ambayo inaweza kujitokeza ni makundi kuwa mengi jambo ambalo linatishia amani ya nchi yetu iliyodumu kwa muda mrefu.
#Lindiicon🇹🇿