Kila kishkwambi cha Sensa kilipaswa kiwe na powerbank yake, lakini hali ni tofauti

Kila kishkwambi cha Sensa kilipaswa kiwe na powerbank yake, lakini hali ni tofauti

Jerlamarel

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
843
Reaction score
2,525
Kulingana na bajeti ilivyopangwa, ni kwamba kila kishkwambi kilipaswa kiambatane na powerbank yake. Lakini makarani wengi waliopo mitaani hasa maeneo ya mijini hawana hizo powerbank.

Kila wakifika kwenye kaya inabidi waombe kufanya kazi yao wakiwa wamechomeka vishkwambi kwenye umeme.

Kumbuka hivi vishkwambi vina betri hafifu yenye 3000mAh tu, ambazo hazidumu hata masaa 5 maana inabidi muda wote kishkwambi kiwe online na kwa sababu matumizi ni full time.

Sababu kubwa kwa nini hawakupewa powerbank ni eti "Ninyi mko maeneo ya mjini hamuhitaji powerbank". Sasa hapo unajiuliza kama mlijua maeneo ya mjini hawatahitaji powerbank kwa nini mlizijumlisha kwenye bajeti? Hizo pesa za hizo powerbank ambazo hazijanunuliwa zimeenda wapi na kwa matumizi gani?

Huenda hii sensa ndiyo itakayovunja rekodi ya ufisadi mkubwa kuwahi kufanyika hapa nchini. Maana kwenye kila sehemu watu wamepiga panga.​
 
Back
Top Bottom