Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
KILA KITU KINACHOTOKEA NI UHALISIA ULIOCHELEWA "DELAYED REALITY"
Tumekuwa tukihamasishwa mara kadhaa kutokuwa watu wa kuongozwa na matukio( matokeo) na badala yake tumeshauriwa sana kuwa watu wanaoona tukio katika uumbikaji wake kabla halijatokea kwa sababu likishatokea tu linakuwa "uhalisia iliochelewa".
Wapo wanaoshauri juu ya kuwa watu wa kuona zaidi ya kuona kwa kutumia macho.Tunalazimika kuona kwa kutumia akili kabla ya kutumia macho "proactive" kwa sababu kuona kwa kutumia macho ni kuchelewa kuona "reactive" na hapo ndipo linapokuja suala la kuchelewa kuona "delayed reality".
Uhalisia uliochelewa huthibitika kwa wengi na kujenga uhalali mkubwa kuliko uhalisia katika uumbikaji wake. Kuchelewa kuona ni pumbazo na liwazo kwa akili za wengi. Hali hii husabanisha pia madhara makubwa kwa wengi.
Hakuna kitu kinachotokea katika ulimwengu wa vitu kwa kuwahi. Yatokeayo yote ni mambo yaliyochelewa kwa sababu ni mambo yaliyotokea tayari katika mawanda ya uumbaji. Siyo ajabu mtu kuota ndoto na ikatokea kutoka maisha yake kama alivyoiota au kwa ufanano mkubwa kutokana na ukweli kuwa mambo mengi hufanyika kikamilifu kabla hatujayaona katika ulimwengu wa vitu.
Kutokana na uhalisia kuchelewa katika ulimwengu wa vitu wapo wanaofanikiwa kuona mapema lakini changamoto wanayoipata ni kukiwasilisha kwa ambao hawajaona. Eneo hili la uhalisia uliochelewa limesababisha kuibuka kwa watu wengi chini ya mwamvuli wa unabii.