Lakini....Ni elimu ndiyo itaifungua nchi yetu kutoka kifungo cha ujinga na umaskini
Ni elimu ndiyo msingi wa maisha na maendeleo
Ni elimu ndilo chimbuko la viongozi weledi na wenye mafanikio nchini.
Mungu awe nanyi katika mwaka mzima huu wa masomo.
Nawapenda watoto wote wa kitanzania.
Kila la kheri.
Dah! Kweli tuna safari ndefu mno yenye kiza kikuu. Wakati watoto wenzao wanajifunza kwa vitendo shughuli wanazoweza kuja kufanya wakimaliza masomo i.e. wanakuza vipawa vyao vya kuwawezesha Ukubwani; sisi wakwetu wanajizoeza kwa bidii sana kukata mauno na kucheza ngoma na mwl. wao amechuchumalia hilo ili lifanikiwe. Lahaula!. Halafu hakuna mbongo anayemshtua mwenzake. Wao wanatutazama kwa mbali wanacheeeeeka. Wao upande wa kushoto wa vid.clip hapo juu Wanajiandaa kwani wanajua iko siku watarudi huku kututawala tena (ukoloni) ila safari hii sio kwa nguvu bali tutawaita ss wenyewe kwa hiari yetu na pengine kwa kuwabembeleza. Ni aibu sana.Lakini....
View attachment 3200289
Hahahaa. Hapo sasa. Dogo anamwambia baba yake: "Dady please, I can't go on my own without u driving me there"Kuna mmoja hapa anataka nimfikishe hadi kwa mwalimu wake .Kazi ipo.