Kila la heri Simba SC. Tanzania kwanza

Kila la heri Simba SC. Tanzania kwanza

SALOK

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
3,364
Reaction score
2,001
Leo Simba SC, wahuni wa pale mitaa ya kati katika mitaa ya Msimbazi, watajaribu tena bahati yao kuwania nafasi ya kushiriki hatua ya Robo Fainali katika Ligi ya Club Bingwa Afrika.

Leo watakipiga katika dimba la nyumbani Uwanja wa Benjamini Mkapa, wakiwakaribisha vibonde wenzao katika kundi lao, Vipers SC.

Kiushabiki nisingepaswa kuwatakia heri hata kidogo Simba SC katika mchezo wa leo, ila natanguliza kwanza uzalendo kwa taifa langu Tanzania.

Simba ni ndugu zangu tena wa damu kabisa (binti yangu wa kwanza ni Kolo FC, mjinga sana huyu mtoto pamoja na mama yake, haahaa), Simba ni rafiki zangu na watani wangu, kila la heri katika mchezo wa leo.

Tanzania kwanza!

NB: Ikitokea mkapoteza mchezo kwasababu za ubovu wenu sitahusika na huzuni, furaha ya kishabiki itachukuwa nafasi yake na haitajalisha mmekung'utwa goli ngapi hata ikiwa mmechapika Manchester kwa nunge!
Simba_Sports_Club.png
Vipers_SC_logo.png
 
Mbona mapema sana, hata chai haijashuka vizuri
 
Huyu kifutu (vipers) leo aoneshe makeke yake tumwelewe vizuri.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Vinginevyo waache kumdhalilisha huyo nyoka mfupi, asiye na hasira za haraka, mwenye sumu yenye kuuwa ama kuacha ulemavu wa kiungo mhanga asipopata tiba mujarabu tena kwa wakati sahihi...
 
Back
Top Bottom