Kila la heri walimu mlio safarini kwenda kuripoti sehemu za kazi

Kila la heri walimu mlio safarini kwenda kuripoti sehemu za kazi

chung cho

Senior Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
191
Reaction score
42
Kwanza hongereni kwa kupata ajira najua ni mwanzo mpya wenye baraka na utajiri mliokusudiwa na Mungu nyinyi ni viungo tegemezi kwa kila aliyefanikiwa na pasipo mwalimu hakuna aliyeweza kuitwa mtu.hata ukiangalia rais wa kwanza tanzania aliitwa mwalimu na mtu aliyekuja kukomboa ulimwengu yaani Yesu aliitwa mwalimu simameni imara nchi itafika mahali itatambua umuhimu wa mwalimu japo kwa sasa walishaanza kupuzia maagizo ya mwalimu nyerere lkn bado hakujaondoa umuhimu wa mwalimu hapa duniani.Mungu awafanikishe mwendako
 
Msisahau kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa ajili ya maisha yenu ya leo kesho na kesho kutwa.
 
Mh! LAPF! Ndio mfuko gani huo. Kwa waalimu PSPF ndio kila kitu. LAPF inawafaa watumishi wa Local government.
 
Mh! LAPF! Ndio mfuko gani huo. Kwa waalimu PSPF ndio kila kitu. LAPF inawafaa watumishi wa Local government.

Ukishafika sehemu husika kila mfuko utaelewesha juu ya mifuko yao nawe utaamua utakacho.
 
Msisahau kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa ajili ya maisha yenu ya leo kesho na kesho kutwa.

unaweza kujiunga na mfuko wowote ule unaoupenda iwe PPF(PARASTATAL PENSION FUND),PSPF(Public service pensions fund),LAPF (local authorities pension fund),NSSF(national social security fund),n.k angalia faida za kila mfuko ndio ujiunge mkuu
 
kanuni ya kukalculate mafao ya PSPF, miezi ya kufanya kazi x mshahara x 100 gawanya kwa 540 ,
 
msidanganyike wadogo zangu PSPF ndo mfuko pekee utakaowafaa msije kujuta baadae HONGERENI SANA
 
Kunahalmashauri mtakuta fomu za LAPF zipo Tayari mnapewa msikubali. Hii ya kuwaelimisha kila mfuko ni sawa lakini haifanywi wanawatawapa fomu
 
Mara pspf, lapf, tunachanganyana.

Mada inazungumzia kuwaombea heri walioko safarini kuelekea kuripoti sehemu zao za kazi.

Anzisheni sredi inayo husu masuala ya pensheni ili tuulize mengi na mtujuze mengi.
 
hongereni mliofika salama.. wengine bado tunaitafakari safari
 
Bon voyage walimu wote mkajenge taifa huru na mfundishe kwa uadilifu Mkubwa.
Binafsi nawapenda walimu without you I wouldn't kick it like this.
 
ahsante mkuu japo tumefika wilayani lakini bado kitendawili hakijateguka ni yapi makazi ya kudumu ni mpaka hapooo j4 eee mungu tusaidie
 
ahsante mkuu japo tumefika wilayani lakini bado kitendawili hakijateguka ni yapi makazi ya kudumu ni mpaka hapooo j4 eee mungu tusaidie

Mpaka hapo ulipofikia ameshafanya njia tayari so patience is of essence
 
Back
Top Bottom