Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Kuna maneno matatu ambayo ni vigumu sana kuyatenganisha, hata kuyaelezea maana yake ni vigumu kumaliza bila kuhusianisha na neno au maneno mengine kati yake. Maneno haya ni RUSHWA, UBADHIRIFU na UFISADI.
Nataka kujikita zaidi katika dhana ya UFISADI. Nitaeleza kwa ufupi maana ya neno Ufisadi, kwa mujibu wa Wikipedia ya Ufisadi: Ufisadi ni upotoshaji au utumiaji mbaya wa mchakato au mwingiliano na mtu mmoja au zaidi kwa madhumuni ya kupata faida fulani kama vile upendeleo maalum. Kwa ujumla tabia hii hupelekea kujitajirisha mtu binafsi au kikundi fulani. Inaweza kumhusu mtu yeyote anayefurahia mamlaka ya kufanya maamuzi, awe mwanasiasa, afisa mtendaji mkuu wa kampuni binafsi, daktari, msuluhishi, na kadhalika.
Kielelezo Na. 1: Ramani ya Dunia inayoonyesha Nchi na Kiwango cha Rushwa, 2022
Chanzo: https://en.wikipedia.org/wiki/Corruption_Perceptions_Index
Kwa mujibu wa kielelezo Na. 1 hapo juu, Tanzania inaangukia kwenye rangi karibu na nyekundu (alama kati ya 30 – 39) katika kiwango cha rushwa, ukilinganisha na nchi zenye rangi ya kijani (alama 80 na kuendelea, ikimaanisha kiwango kidogo zaidi cha rushwa). Tukiimarisha Uwajibikaji na Utawala Bora, tuna nafasi ya kufikia rangi ya kijani!
Kwa mujibu wa maelezo hapo juu, utaona namna ambavyo yale maneno mengine (RUSHWA na UBADHIRIFU) yanavyoingia ndani ya ufisadi. Maana yake ni kwamba, huwezi kuwa Fisadi bila kuhusika na kutoa au kupokea Rushwa, na pia bila kufanya Ubadhirifu (Matumizi mabaya ya mali ya mtu mwingine au ya umma). Na hii ndio sababu awali nimesema ni vigumu sana kutenganisha maneno haya matatu, yaani RUSHWA, UBADHIRIFU na UFISADI!
Inasikitisha sana kusikia habari za ufisadi katika sekta mbalimbali za umma kila mwaka katika enzi ambayo mifumo ya uwajibikaji na hasa kwa kutumia TEHAMA inazidi kuimarishwa.
Kwani kwa mujibu wa Sauti ya Amerika (March, 2023), kwa mara nyingine tena ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inaonyesha upotevu wa fedha za umma, jambo ambalo linaashiria kiwango kikubwa cha ufisadi unaofanyika katika baadhi ya mamlaka na taasisi za umma.
Kwenye ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 aliyoikabidhi kwa Rais Samia hapo Machi 29, 2023, CAG Charles Kichere alibaini mambo kadhaa yanayohusiana na usimamizi usio sawa wa fedha za umma.
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya mwaka 2023, Mashirika ya umma ya kibiashara 14 yalipata hasara katika mwaka wa fedha 2021/2022, miongoni mwa hayo ni shirika la ya Ndege la Tanzania ATCL lililopata hasara ya Tsh. Bilioni 35.2 na Shirika la Reli TRC lillilopata hasara ya Tsh. Bil 31.2.
Akichangia kwenye mjadala huo uliofanyika katika hoteli ya Four Points, CAG mstaafu Ludovick Utouh alisema kwamba ifike mahala watendaji wanaobainika kuwa wabadhirifu wachukuliwe hatua kali za kisheria badala ya kuhamishiwa kwenye idara nyingine za Serikali. Pendekezo kama hili liliwahi kutolewa na CAG mstaafu Profesa Mussa Assad.
Njia nyingine ambazo Utouh amependekeza na ambazo anaamini kama zitatekelezwa zitasaidia kudhibiti ubadhirifu Serikalini ni nafasi za wakuu wa mashirika ya umma yenye lengo la kuzalisha faida zipatikane kwa njia za kiushindani badala ya uteuzi kama ilivyo hivi sasa.
Napenda kupigia mstari pendekezo hili kwa maana nafasi nyingi za uteuzi hazizingatii ujuzi na ueledi wa wahusika, bali ni ukaribu au uhusiano na mtu au watu wenye mamlaka ya kufanya teuzi.
Kama Wakuu wa Mashirika au Taasisi za umma wapo karibu na yule au wale wanaowateua, wakiharibu kazi, inakuwa vigumu sana kuwajibishwa kwa wakati, na badala yake tumeshuhudia baadhi yao wakiharibu shirika moja, badala ya kuwajibishwa kisheria, wanapelekwa mashirika au taasisi nyingine.
Utamaduni wa upigaji
Pengine kinachowauma wananchi walio wengi ni kuona ni kwa namna gani ripoti zilezile za ubadhirifu wa kupitiliza zinaripotiwa na CAG kila mwaka kwenye taarifa zake za ukaguzi.
Hali hii ya kujirudia kwa taarifa hizi imewafanya baadhi ya wadadisi kuhoji endapo kama ufisadi unatokana na udhaifu wa Serikali au ni sehemu ya tatizo pana la kijamii? Akiandika kwenye “The Chanzo” kuhusiana na ripoti ya CAG kwa mwaka 2020/2021, mchambuzi Njonjo Mfaume alisema ubadhirifu Serikalini ni matokeo ya kuwa na jamii inayotukuza ufisadi. “Jambo la msingi hapa ni kuwa vita dhidi ya ufisadi na rushwa lazima ipiganwe kwa mbinu tofauti,” aliandika Mfaume, akisisitiza umuhimu wa elimu kwa umma. “Ni kurahisisha tatizo gumu na kujidanganya kudhani kuwa ukali wa viongozi pekee utaondoa ufisadi.”
Semkae Kilonzo (Machi, 2023) alibainisha kwamba vita dhidi ya ufisadi haiwezi kukoma kwa kufukuzwa kwa mtendaji wa idara fulani tu. “Kuna mifumo pale na wataalamu wa kucheza na mifumo ni wale waliopo chini. Kuna utamaduni fulani hizi taasisi za umma wa kusema kwamba watakaowajibishwa ni wale waliopo juu, wenye dhamana za kisiasa, sisi huku huwa hatuguswi,” aliongeza.
Madhara ya Ufisadi katika Taasisi za Umma
Serikali iwe inachukuwa hatua za kisheria haraka (isizidi wiki moja) mara baada ya kupokea taarifa za ukaguzi wa mahesabu, ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ubadhirifu kuwa chini ya ulinzi pamoja na mali zao wakati uchunguzi wa kina ukiendelea, na hatimaye wafikishwe mahakamani.
Marejeo
Ufisadi - Wikipedia, kamusi elezo huru
Je, Ubadhirifu Serikalini Unaweza Kudhibitiwa? Wataalamu Wanaamini Hivyo - The Chanzo
Mafisadi Tanzania wawajibishwe

- Serikali ina matumizi mengi, ikiwa ni pamoja na kugharamia Bunge, Mahakama, uendeshaji wa serikali yenyewe, miradi ya kimkakati (kama reli, barabara, umeme, na kadhalika). Panapokuwa na upotevu wa mabilioni ya fedha kila mwaka katika taasisi zilizopaswa kuchangia gharama hizi, ndipo serikali huhamia katika maeneo manyonge ya kukusanya mapato ambapo watu wa kawaida hulazimika kulipa kodi zaidi aidha moja kwa moja au kupitia ongezeko la kodi kwenye bidhaa mbalimbali zinazotumiwa na watu wengi wa kawada (au wa kipato cha chini).
- Mzigo wa madeni ya nje huongezeka kila mwaka, ili kufidia pengo linalosababishwa na upotevu wa fedha katika taasisi hizi.
- Kutokana na tabia ya serikali kuongeza kodi kila mara katika bidhaa muhimu, mfumuko wa bei hushuhudiwa karibu kila mwaka, jambo linalofanya Maisha ya wananchi wengi kuendelea kuwa magumu.
- Nafasi za Uteuzi ziondolewe, na badala yake ziwekwe kwenye ushindani ili wapatikane watendaji wenye ujuzi na ueledi stahiki.
- Taasisi au Mashirika yanayopata hasara, aidha yafungwe au yabinafsishwe.
- Elimu ya Uadilifu, Uwajibikaji na Uzalendo itolewe kwa umma, ikianzia mashuleni.
- Serikali itumie wataalam wa TEHAMA, waliopo serikalini na walipo nje ya serikali kutengeneza na/au kuimarisha mifumo ya uwajibikaji katika kila idara, ili hatimaye mianya yote ya RUSHWA na UBADHIRIFU izibwe kabisa.

Upvote
7