Kila mnyonge ana mnyonge wake

Kila mnyonge ana mnyonge wake

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Picha linaanza bhana Baada ya boss KUMFOKEA manager

Manager naye Anaona isiwe kinyonge anashuka kwa MA-operator anaowasimamia anaanza KUMFOKEA operator mmoja wapo!

Operator anafanya kazi huku anajaziba ya kufokewa na manager

Operator anarudi na hasira nyumbani na kilo za nyama wife akampikie rost fulani ajipoze hasira😋 mida ya Kula inafika kimbe wife naye kazidisha chumvi kwa mboga anamfokea wife wake

Wife nae anapata hasira mara watoto wanamwaga mwaga chakula chini wife anahamashia anamalizia hasira kwa watoto anawachapa watoto wanapata hasira

Watoto nao wanachukua makombo ya nyama yaliyobaki wanapeleka kwenye banda la mbwa,mbwa hataki kula wanachukua fimbo wanamtandika mbwa 😂mbwa anapata hasira

Paka inapita kuramba Yale makombo🤣mbwa annamrarua paka kwa hasira

(kiufupi Kila mnyonge Ana mnyonge wake kazi iendelee)
 
ongeza na hii, wanafunzi wanatakiwa kupiga picha, mwl mkuu anamtafuta mpiga picha wanakubaliana bei ni sh. 1500, mwl anatoa maagizo kwa walimu wa madarasa anawaambia picha ni 2000 kila mwanafunzi, walimu wa madarasa wanwatangazia wanafunzi kuwa kila mwanafunzi alete 2500 kwa ajili ya picha, naye mwanafunzi anaenda nyumbani anamwambia mama yake shuleni mwl amesema tupeleke 3000 kwa ajili ya picha, Naye mama anafikisha kwa Baba na kumwambia shuleni watoto wameagizwa wapeleke 4000 kwa ajili ya kupiga picha.

Baba atatoa 5000
 
hii kitaalam tunaiitaje mkuu!
 
Back
Top Bottom