Kila mtu analalamika nchi hii: Ukingo wa kujiliwaza dhidi ya makosa na kukwepa uwajibikaji

Kila mtu analalamika nchi hii: Ukingo wa kujiliwaza dhidi ya makosa na kukwepa uwajibikaji

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Katika hali inayoumiza na kusikitisha ni namna tunavyoyajadili masuala makubwa ya Taifa letu. Nimepitia maandiko mengi, mijadala mingi na hotuba kadhaa ila nilichokibaini nimekipa jina mchezo wa lawama "blame game". Inaweza kuonekana kama lugha kali kidogo kwa wakubwa ila hakuna lugha nyingine ya kusema ukweli zaidi ya kupokea maumivu ya ukweli yalivyo.

Kila upande unalalamika kwa kiasi kikubwa kuliko kuwajibika. Inumiza sana pale tunaposahau kabisa misingi ya uwajibikaji na kukimbilia kujitakasa dhidi ya makosa na kuukwepa wajibu wetu kwa sababu zozote zile. Leo tumefikia mahali ambapo kupata sababu chanzi root-causes ni vigumu mno kutokana na mtindo tuliouchagua wa kujitakasa, kujitafutia pumbazo la kukwepa uwajibikaji comfort zone badala ya kuwajibika na kukubali haswa kuwa sisi wenyewe ni sababu pia ya hali ilivyo.

Ni kama kila mtu ananawa na kumwagia mwingine maji machafu hivi. Hali hii hakika haitatusaidia hata kidogo zaidi ya kuudhohofisha kabisa tabia ya uwajibikaji wa wa pamoja juu ya masuala yanayogusa maslahi ya Umma.

Tumekimbilia sana kutafuta sifa za umalaika kuliko sifa zetu za ubinadamu. Badala ya kuwajibika tunajitetea na kutumia mtindo wa kujitetea kama njia ya utatuzi wa kero mbalimbali zinazotugusa mtu mmoja mmoja au Taifa kwa ujumla.

Tunajenga msingi mbaya sana utakaotugharimu siyo sisi tu ila vizazi kadhaa vijavyo. Tunapochagua hatua ya kukimbilia mahali pa kujificha ili kukwepa kuwajibika ni dhahiri tunatengeneza njia hatari sana ya utatuzi wa changamoto zetu.

Tunapojificha chini ya itikadi fulani au mlengo fulani wa namna yoyote ile kwa maslahi binafsi na siyo maslahi mapana ya kitaifa ni ukweli usiyo na shaka kuwa kero za jamii pana hazitapata suluhu zaidi ya kupoozwa tu.

Kwa mtazamo wangu, yapo masuala ambayo tunapaswa kuwa na akili huru "open minded" tunapoyajdili na zaidi sana kuweka lol aina ya maslahi binafsi pembeni Ili kuweza kuyapatia suluhu. Taifa letu linahitani mijdala huru zaidi kuliko ile inyofungamana itikadi za nmna yoyote wakati huu kuliko wakati wowote ule.
 
Back
Top Bottom