GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Wanasema, mpe mbwa mzee jina zuri! Anaweza asiwe na uwezo wa kuwinda, lakini kutokana na kupewa jina zuri, atajitahudi kuliishi hilo jina.
Mwaka Jana, nikiwa mkoa fulani, nilitaka kumpa mzee mmoja kikazi fulani sehemu nilikokuwa nikifanyia shughuli zangu. Kusudio langu halikufanikiwa kwa sababu huyo mzee alinionesha jeuri fulani hivi. Alikuwa akinijibu kwa kiburi, hivyo na mimi nikaamua kuachana naye. Nilishajaribu kutaka kumpa hiyo kazi zaidi ya mara moja lakini sikufanikiwa.
Huyo mzee anaishi jirani na ulipo mradi wangu ilhali mimi ni wa mkoa mwingine. Huwa ninapatembelea mara chache.
Kipindi fulani mwaka huu, nilipata fursa ya kutengeneza naye ukaribu. Siku moja, nilimtembelea kwenye "kibanda" chake anachoishi na kupiga naye stori. Tuliongea kwa muda mrefu, yeye akiwa ndiye mzungaji mkuu. Tuliongea mpaka nikaamua kusitisha mazungumzo, vinginevyo, labda tungeongea mpaka Usiku. Ilikuwa kama vile alikuwa na njaa ya kumpata mtu wa kupiga naye stori.
Kupitia mazungumzo ya siku hiyo, nilibaini kuwa ni Askari Mstaafu wa JWTZ, tena aliyepigana vita vya Uganda/ Idadi Amin, ingawa maisha yake kwa sasa si mazuri kiuchumi. "Kapigika"
Kuanzia siku hiyo, nilianza kumwita "kamanda", jina ambalo alionekana kulifurahia sana. Kumwita kwangu hivyo kulimfanya awe kama rafiki yangu, kiasi kwamba wakati mwingine, ninapoenda huko, wakati wa kuondoka huniomba nimpelekee vitu fulani kutoka mjini. Hakuwa na uhuru wa kuniambia mambo kama hayo siku za nyuma. Ujasiri huo kaupata baada ya kuwa "rafiki" yangu, urafiki uliochochewa na jina "kamanda".
Siku chache baadaye, nilimwomba awe ananisaidia kazi fulani halafu mwishoni mwa mwezi niwe nampa hela ya "vocha", jukumu ambalo alilikubali kwa mikono miwili, ingawa malipo ni "kidunchu".
Nini kimembadilisha?
Jina zuri, "Kamanda".
Watu, kwa kawaida, hujitajidi kuyaishi matarajio ya watu waliowakubali maishani mwao. Hiyo ndiyo inayochoches baadhi ya vijana wenye marafiki wanaotumia madawa ya kulevya nao kuangukia kwenye hilo janga. Hawafanyi hivyo kwa kupenda, bali wanataka kukubalika kwenye group lake.
Kila mtu anataka atambulike kuwa ni "somebody". Utafanya vizuri ukiwatambua kiusahihi wanaokuzunguka na hata unaokutana nao.