Kila mtu awajibike badala kisingizio cha simba inapendelewa kuwa kichaka cha kuficha wanaofeli majukumu yao

Kila mtu awajibike badala kisingizio cha simba inapendelewa kuwa kichaka cha kuficha wanaofeli majukumu yao

hizi rushwa michezoni takukuru wanazichekea sijui kwa nini, watu mnaingia uwanjani mnajua kabisa refa kaongwa
 
Kambuzi na wenzie wameondolewa kwa kupata alama za chini katika uchezeshaji. Kuna tofauti kati ya kutomudu mechi na kupendelea timu moja. Tena nasema Kambuzi ameponzwa na waamuzi wasaidizi uwezo wao ulikuwa wa chini sana.

Penati zote halali kabisaaaaaaaaaaa
 
HATUWEZI kuwa na timu ambayo zinapendelewa halafu tukafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa. Kama tutakuwa na ligi yenye kiwango sahihi, basi tuna kila sababu ya kuwa na timu imara.


Kama Ligi Kuu Bara ina timu 20, tunaamini kumekuwa na ushindani mkubwa katika mechi nyingi hasa zile zinazoonyeshwa kwenye runinga ya Azam TV ambayo tunapaswa kuipongeza kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye mpira wa Tanzania baada ya mechi nyingi kuanza kurushwa moja kwa moja.


Umesikia watu wengi ambao ni wadau wa karibu kama wachezaji, makocha na kadhalika wamekuwa wakisema kuwa mechi nyingi zinazoonyeshwa moja kwa moja huwa hazina upendeleo.


Wanasema mechi nyingi zisizoonyeshwa, timu wenyeji wamekuwa wakipewa upendeleo wa wazi kuhakikisha wanabeba pointi za nyumbani maana yake si kwa uwezo wa mpira, jambo ambalo ni bayana linaudumaza mpira wa Tanzania ambao tunaupigania kukua.


Ili soka likue, lazima liwe na haki na nafasi kwa watu kuchezeshwa kwa haki, haki itawale na kutengeneza uimara unaotokana na ushindani sahihi kabisa.


Nimeamua kuandika makala haya baada ya kuona kuna kampeni ya chinichini ambayo haina faida kwa mpira wa Tanzania na inaonekana tumekuwa tunaoneana haya kwa kisingizio cha fulani shabiki wa timu fulani.


Kampeni za kusema Simba inapendelewa, Simba imekuwa ikipewa nafasi ya kushinda na kadhalika. Lakini wanaosema wamekuwa hawana uthibitisho wa zaidi ya asilimia 90 wa wanayoyasema.


Kinachoshangaza ni kuona na watu wengine ambao hawajaribu kutafakari yanayozungumzwa, wanayachukua na wao kuyazungumza kutoka kwa waliyoyasikia bila sababu au hoja sahihi.


Simba inapendelewa katika mechi ipi, kama imefunga mabao halali, vipi inapendelewa. Kuna bao ilipendelewa, jibu hapana, ila ilichezeshwa saa 8 badala ya saa 10 kama ilivyoelezwa. Kwani aliyecheza naye alicheza saa ngapi, naye alicheza muda huo pia. Sasa kupendelewa kunatokana na nini hasa?


Sote tunajua, Simba ndio wana timu bora kabisa katika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu na hili linadhihirishwa na takwimu zao kwa maana ya wastani lakini hata hatua waliyofikia kimataifa na kuitangaza Simba mbali barani Afrika.


Pamoja na hivyo, unaona Simba iliyoifunga Al Ahly, AS Vita, JS Saoura na kutoka sare na TP Mazembe, imekwenda kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar ambayo inapambana kuepuka kuteremka daraja katika Ligi Kuu Bara!


Hapo unaweza kujiuliza, kwamba kama ni hivyo, Simba inayopendelewa inafungwa vipi na Kagera Sugar, inahenyeshwa vipi na KMC lakini kabla ya hapo tuliiona ikipata shida kubwa dhidi ya Coastal Union pale Tanga.


Wanaofanya kampeni za kutengeneza lawama ni kampeni chafu na za kipuuzi, kampeni zinazoonyesha wameshindwa kufanya kazi zao na baada ya hapo wanasambaza maneno yatakayowalinda siku wakianza kuhojiwa kutokana na kufeli majukumu waliyokabidhiwa.


Kwa wale mnaosikia, vipi uamini vitu tofauti na ambavyo unaviona. Mtu hadi akuaminishe tofauti wakati na wewe uliona kabisa kila kitu kilivyo, vipi mtu mwingine akuaminishe tofauti na wewe uamini.


Wanaosambaza kile kisicho sahihi, vizuri kuwahoji kwa hoja badala ya kukubali kubeba wanachokisema hata kama ni pumba na kukisambaza pia.


Hatuwezi kuwa tayari kuona timu moja, mfano Simba inapendelewa halafu tukakaa kimya. Lakini kama si hivyo, basi mimi sitakaa kimya ili suala la mechi zinazochezwa tujadili mambo ya msingi na si haya ya kubabaisha kutokana na kuwapinga wanaobabaisha mambo.


Pia haitakuwa sahihi kuwasikia Simba sasa nao wakisema Yanga wanapendelewa baada ya ndani ya mechi tatu, kupoteza na kushinda moja wakati matarajio ilikuwa ni kushinda zote.


Tuache mpira uchezwe na kama kuna malalamiko yawe ya msingi badala ya kusambaza upuuzi.
Si sawa mechi ya juzi CCM kirumba Kati ya KMC na Simba ilivurugwa . Muulize yeyote bila unazi atakuambia na hawakustahili ushindi.

Uzuri wa Simba upo midomoni mwa washabiki si uwanjani. Mechi ya Alliance walishinda halali lakini kwa KMC mwamuzi alikuwa na matokeo mfukoni. I was there and I attended all matches
 
Hili la marefa kuindolewa kuchezesha ligi kuu ndo linafanyika kwa mara kwa mara ya kwanza? Na je wamesemwa kwamba wameondolewa kwa sababu wameipendelea Simba? Yanga imefunfishwa tabia ya hovyo kabisa na Zahera, kulalamika badala ya kuipush timu yao ifanye vizuri. Kwa namna hii ni kama wameshakubali kishindwa na sasa wanajiliwaza kwa kushindwa kwao!
Okwi akimnawisha mtu ni penalty lakini akikamatishwa yeye hadharani siyo penati !! Mechi Ile refa aliharibu na ndiyo maana amechukuliwa hatua mara moja.
 
Kambuzi na wenzie wameondolewa kwa kupata alama za chini katika uchezeshaji. Kuna tofauti kati ya kutomudu mechi na kupendelea timu moja. Tena nasema Kambuzi ameponzwa na waamuzi wasaidizi uwezo wao ulikuwa wa chini sana.

Penati zote halali kabisaaaaaaaaaaa
Na penalty ya okwi kupanchi mpira kwa mkono si halali siyo ?!
 
Hivi nani alisema Refa alipuliza filimbi ya offside baada ya ile video.??mlijuaje kama ni offside??Mimi niliona beki wa Simba alipiga mpira ukambambatiza forward wa KMC mkononi ndio refa akapiga filimbi.Wekeni video
Kwa nini marefa wameondolewa.
Zahera kaitwa Takukuru mtaenda kuelezea wachezaji wa SINGIDA, JKT na timu nyingine nani alikuwa anawapa 10m
 
Ahahahaaaa [emoji12][emoji3][emoji23][emoji1787][emoji1787] I was there sir !! Ilikuwa aibu. Hamkustahili kushinda Ile mechi .

Kutokustahili kushinda na mpira kugonga mbavu ni vitu viwili tofauti. Marudio ya Azam TV yako very clear, mpira uligonga mbavuni mwa Okwi, ila ninyi mnalazimisha kwamba mtu alishika. Unless uniambie Azamtv wame-edit video
 
mficha uchi hazai, bila kupindisha maneno inabidi mo-dewji na magori waapewe makavu live bila chenga kuwa 'wanayo yafanya' si sawa kwa maendeleo ya football la TZ ingawa yanaweza kuwa sawa kwa simba kwa kiasi flani na kwa muda flani!
 
Kutokustahili kushinda na mpira kugonga mbavu ni vitu viwili tofauti. Marudio ya Azam TV yako very clear, mpira uligonga mbavuni mwa Okwi, ila ninyi mnalazimisha kwamba mtu alishika. Unless uniambie Azamtv wame-edit video
Mimi nilikueko stadium na je backpass unaizungumziaje ?!. Refa alifanya madudu mengi. Na alionyesha mapema anatakaje
 
HATUWEZI kuwa na timu ambayo zinapendelazembe, imekwenda kufungwa
Tuache mpira uchezwe na kama kuna malalamiko yawe ya msingi badala ya kusambaza upuuzi.
kuwa na kikosi bora hakuzuii mtu kubebwa mara ngapi tumeona madrid au barcelona wskibebwa japokuwa walikua na vikosi bora kipindi hicho? ni kweli simba ana kikoso bora hilo liko wazi lkn madhaifu madogo madogo yasifumbiwe macho hatuhitaji lawama wala visingizio kwenye ligi km mechi saa kumi basi ichezwe saa kumi na si kuharibu saikolojia za watu kwa kuichezesha mchana au asubuhi nn maana ya ratiba sasa?
 
Tumsubiri Zahera akienda na kurudi Takukuru, maana anaenda kuonesha ushahidi wote kuhusu rushwa anayowapakazia Simba, naskia anavithibitisho hadi vya walivyopewa Yanga kwenye mchezo wao dhidi ya Simba, ambavyo amevitoa kwa Haroub Kanavaro.
 
Back
Top Bottom