HOJA Kila mwaka Wanafunzi kuagizwa kuja na majembe na mafyekeo: Vya mwaka jana huwa vinaenda wapi?

HOJA Kila mwaka Wanafunzi kuagizwa kuja na majembe na mafyekeo: Vya mwaka jana huwa vinaenda wapi?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Mutaajir

New Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
1
Reaction score
3
Kila mwaka shule nyingi za serikali huwa zinawaagiza wanafunzi kuja na vifaa kama majembe, mafyekeo, ndoo, mifagio na vifaa vingine vya usafi.

Swali langu ni hili; ikiwa maagizo haya yanatolewa kila mwaka kwa wanafunzi wapya na hata wanaorejea shuleni, je, vifaa vya mwaka uliopita huwa vinaenda wapi?

Je, vinaisha matumizi ndani ya mwaka mmoja, vinaharibika kwa kiwango kikubwa, au kuna mfumo gani wa usimamizi na uhifadhi wa vifaa hivyo? Pia, je, shule huwa zinafanya tathmini ya vifaa vilivyopo kabla ya kuwaagiza tena wazazi kununua vingine?

Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kupunguza gharama za elimu kwa wazazi, lakini upande mwingine wazazi wanaendelea kubeba gharama hizi za vifaa kila mwaka.

Hivyo ni muhimu kuwepo uwazi zaidi kuhusu matumizi, uhifadhi na hatima ya vifaa hivyo ili kuhakikisha kuwa maagizo yanayotolewa yanatokana na mahitaji halisi ya shule na si kuongeza mzigo wa gharama kwa wazazi.

Wadau, walimu na viongozi wa elimu, mnaonaje suala hili? Je, utaratibu huu ni wa lazima kutokana na uhalisia wa matumizi ya vifa
 
Ulisoma Shule gani Mkuu?

Kujibu hoja yako
1. Vifaa hivyo hua vinaharibika sana, kutokana na watoto wenu kuto kujali mali za umma.

2. Sio wote wanao leta hivo vifaa, wapo wanafunzi ni manunda wana kaza mqanzo mwisho hawaleti.

3.Wizi wa vifaa kwa wanafunzi na wanakijiji.

4.Shule nyingi ni mwaka wa kwanza tu wanakuja na vifaa hivyo, miaka mingine wanatumia vilivyo letwa na mwaka wa kwanza/Form one.
 
Wanafunzi watukutu tunaviibaga kidogo kidogo, vingine tunaviacha machakani, msimu unaokuja ukifika vinakuwa vinapungua au vinaisha kabsa kutokana na idadi ya wanafunzi watukutu

Binafsi nilichukuaga panga.. nikarudigi nalo nyumbani .. nilichukua sikuibaga

Ila ukweli ndio huo, wanafunzi watukutu wanayaiba na kurudi nayo nyumbani wengine wanayauza mitaani

Mbande, mvuti, msongola, mbondole secondary school wananielewa
 
Eeeeh ndio mmeamua kututaja ili tuone aibu? Alisema hadi mwakani jamani!!!

Vinapotea na kuharibika bwana. Vingine mnaiba nyie nyie wanafunzi. Hivyo endeleeni tu kupeleka vingine.
 
Back
Top Bottom