shavu kubwa
Member
- Jun 13, 2016
- 25
- 32
Habarini ndugu wana jamii forum, mimi si mwenyeji sana na pengine ni mara yangu ya kwanza kupost kwenye jukwaa hili:
Kwa kuanza: kuna dhana ya watu wengi hivi sasa kuishi kwa kutegemea miujiza kuliko kufanya kazi na kujiletea maendeleo, hii nimeiona hata pale mikutano ya kiinjili inapotangazwa watumishi wengi wanapenda kusema maneno haya.
Karibu kwenye mkutano flani upokee muujiza wako, je umeachika na mme na unahitaji arudi, je umehangaika kutafuta kazi bila mafanikio, nk.
Ambapo humo pote wanagusa matatizo yaleyale ya mwanadamu ya kila siku, sasa tuliowengi kwa ufinyu wa fikra kila tukiona mkutano wa injiri tunakimbilia kwa kutegemea miujiza, ukisikia kwingine tena unakimbilia ukitegemea maisha yatabadilika kwa mfumo huo.
Kiukweli na uhalisia ni kwamba mungu yupo ndani ya kila mmoja wetu ni kitendo tu cha wewe kutenga muda wako vizuri na kumuomba hata hapo hapo nyumbani kwako utaona majibu yake, mungu hajawaki kutoka ndani yetu na kukimbilia kwa mtu mmoja tu ili tuwe tunamfuata huko kutatua matatizo na shida zetu.
Kitu kingine cha ziada ni kuhusu hii mikutano ya injili ya siku hizi ambapo wameingia na matapeli humohumo ambao wanatumia neno la mungu kwa kujinufaisha na bado watu hawastuki, mi nafikiri watu hao wengi wao ni wafinyu wa mawazo wanaofikiri maisha yao yatabadilika kwa kwenda kumtafuta mungu kwa mtu mwingine wakati wewe mwenyewe unae na ndio huyo huyo, lakini pia watu hawajishughulishi katika kutafuta zaidi na inafikia watu wanashinda tu kanisani from monday to sunday jamani tubadilike.
Kitu cha kujiuliza ulishawahi kumuona kilema unaemfahamu kabisa jirani yako kaenda kuombewa akapona ulemavu wake, mi naona vingi vinavyofanyika katika mikutano baadhi ni viini macho tu na watu wengi wanakuwa wameandaliwa tayari
Ukweli kabisa mungu unae wewe mwenyewe ndani yako, ukitaka kujua amka usiku wa manane wakati ambao kichwa kinakuwa kimetulia kabisa na hakuna kelele ya aina yoyote halafu jongea mbele za mungu kwa njia ya maombi na utaona majibu yako katika kila unaloomba, fanya hvyo kila wakati.
Itaendelea
Nakaribisha maoni zaidi ya wadau