Riadha hutegemea na bidii ya mtu binafsi. Ukiangalia mikoa yote, sote tukiwa wadogo kule shuleni, tulikimbia sana. Hata leo, watoto wengi wanakimbia sana tena mikoa yote. Lakini kadiri wanavyoanza kukua watu wazima, ile bidii inabadilika kulingana na mazingira kwa kukosa hamasa.
Mimi kwetu Ukikuyuni, yaani jamii ya Wakikuyu ni kama Wachagga vile, ukikua unawaza sana mambo ya biashara na kutengeneza hela. Unakuta tukiwa wadogo tunafanya vizuri sana kwenye riadha, lakini baada ya kukua watu wazima, wachache sana tunaendeleza riadha. Wengi tunaishia kwenye biashara za maduka, ujasiria wa kila aina. Lakini pia kuna baadhi ya hao Wakikuyu ambao wanadumisha utashi wa michezo, na wanaendeleza hiyo bidii hadi kwenye ngazi za kimataifa.
Lakini ukienda bonde la ufa kwa Wakalenjin, wengi wanaendelea na hayo mambo ya kukimbia hadi ukubwani. Barabarani unakuta kundi kubwa la watu wanakimbia wakifanya mazoezi.
Pia ukienda kwa jamii za Wajaluo na Waluhya, utakuta wengi wanapenda sana kucheza mpira katika ukubwani.
Hivyo mtu yeyote anaweza kuwa mwanariadha au mwana michezo, cha msingi ni kufanya maamuzi na kutia bidii, sio lazima uoe eti kwa kabila nyingine ndio utakua mwanariadha, vijisababu vyenu hivyo vya uswazi ni kero aisei.