Uteuzi wa Samia kuwa mgombea wa Urais ulikiuka kila kitu, kuanzia katiba ya CCM na ya nchi, sheria za uchaguzi, mpaka mazoea ya CCM.
UFafanuzi:
1. Magufuli na Samia walizunguka nchi nzima wakiomba kupewamamlaka ya kuunda setikali ya awamu ya 5. Bahati mbaya Magufuli akafariki kabla ya awamu ya 5 kumalizika. Aliyekuwa msaidizi wake akapewa usukani kumalizia awamu ya 5. Awamu hiyo ya 5 ilikuwa na ilani yake ya uchaguzi ambayondiyo ilikuwa mwongozo wa Serikali. Samia alipopewa uongozi akapindua meza na kudai kuwa ni Rais wa awamu ya 6, ina maana sasa ilikuwa ni awamu isiyo na ilani kwani hakuwahi kuitangaza hiyo ilani kwa wananchi kuwaomba wamchague ili akaunde Serikali yaawamu ya 6.
2. Mazoea ya CCM, ni kutomshindanisha Rais na wagombea wengine na hivyo kuifanya awamu kuwa ni kipindi cha miaka 10. Lakini baada ya kumaliza awamu, yaani miaka 10, ni desturi ya CCM kuufanya uteuzi wa mgombea Urais wa awamu inayofuata kuwa huru kabisa. Hivyo, kiuhalisia, baada ya kumalizika awamu ya 5 iliyoongozwa na hayati Magufuli na Samia, ambayo ukomo wake ni 2025, kwa desturi ya CCM, mchakato wa kumpata mgombea wa awamu ya 6, ulistahili kuwa huru kabisa kwa wanachama wote. Lakini Samia ameharibu mazoea hayo ya CCM, yeye binafsi akaamua kujipachika na kujitangaza kuwa ni mgombea pekee.
3. Samia ameharibu hata mpangilio wa awamu kama ilivyozoeleka. Alijitangaza ni Rais wa awamu hewa, awamu ya 6. Na safari hii, sijui anagombea ili awe Rais wa awamu gani!!
NB: Aliyeshimdwa kuheshimu katiba na taratibu za chama chake, kamqe hawezi kuiheshimu katiba ya nchi, wala sheria zake. Na kiongozi asiteheshimu katiba anaweza kugeuka kuwa jambazi dhidi ya wananchi. Ndiyo maana tunashuhudia ujambazi wa ajabu dhidi ya wananchi: kuteka na kuua watu, kuwapoteza watu, kuwajeruhi, na kupora haki mbalimbali za wananchi.
Wahemga walisema, siku njema huonekana tangu asubuhi. Sisi kwa haya tuliyoyashuhudia asubuhi tunapata ujasiri gani kutegemea mchana au jioni itakuwa nzuri?