Kila Nafsi itaonja Umauti,vipi kuhusu mwili unaendelea kuishi?

Kila Nafsi itaonja Umauti,vipi kuhusu mwili unaendelea kuishi?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Kitabu kitakatifu cha Quran Kinatanabaisha kuwa binadamu na viumbe vyengine ni nafsi na lazima vionje(kupitia/mchakato wa kifo).

Swali langu linakuja vipi kuhusu mwili je,haufi?au ndiyo unazaliwa upya baada ya miaka kadhaa(aacording to indian Holly books).

Unapokufa sawa mwili unaachana na roho/nafsi na inakuwaje siku ya mwisho inasemekana kuwa tutarudishiwa miili yetu kwa ajili ya kupatiwa hesabu zetu??je tunakubaliana mwili pia unakufa??
 
Kwa Mujibu wa Bible( Samahani maana Quran tukufu siifahamu sawasawa) Mwanadamu ni Combination ya vitu vitatu. Mwili/ Udongo, nafsi/ pumzi pamoja na roho/Mtu.

Wewe ni mtu/roho na hautakufa. Mwili ni mavumbi tu au housing. Nafsi ni kiunganishi cha mwili na roho yako ili viweze kufanya kazi pamoja.

jibu: Mwili unakufa na haujirudi tena baada ya kupoteza pumzi ya uhai ambayo ni nafsi.
 
unapofufuliwa unarejeshewa mwili inakuwaje hapo?
 
Kila nafsi itaonya mauti ni kauli ya Uongo.
Kuna watu watakutwa hai siku ya kiyama ya watu
 
Back
Top Bottom