Kila nikianza mazoezi ya viungo baada ya wiki mbili au tatu naacha, nikijitahidi mwezi mmoja baadaye naacha

Kila nikianza mazoezi ya viungo baada ya wiki mbili au tatu naacha, nikijitahidi mwezi mmoja baadaye naacha

1kush africa

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
9,552
Reaction score
13,090
Wazoefu mnipe kautaratibu inakuaje mna dumu kufanya mazoezi mwaka mzima bila kuacha? au mnatumia mbinu gani?

MAZOEZI NI AFYA

MREJESHO: Siku kama ya leo ya tarehe 9 jul 2018 ndo nilitoa hii nyuzi,

Leo tarehe 9 August 2018 nimefikisha mwezi mmoja ya tangia nianze mazoezi, Nimeamini ukitia Nia kumbe yawezekana, asanteni sana kwa mawazo yenu.

MWILI UNAENDELEA KUJIGAWA.

[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mazoezi hayana ujuzi kila siku ni mpya... Kama mm uwa ninakimbia kwa wiki Mara 4 muda wa alfaji asubuhi dk 30 Lakin kila ninapo damka alifajiri mwilihuwa unakataa inabidi kujilazimisha.... Ukiweza tafuta mtu mwingine mshawisha na Yeye akipenda mazoezi itakupa motisha Leo ukichoka Yeye atakushawishi hivyo hivyo na Yeye siku Akiwa mvivu uta mvuta... Mazoezi ayazoeleki mkuu ni kudhamiria kwa sasa Mimi Nina mwaka na miezi Sita.. Ninauwezo wa kukimbia bila kupumzika kwa lisaaa pumzi ipo ya kutosha....
 
aiseee shukrani kaka,, naanza ivo ivo lakini uvivu ndo shida, maana siku ya kwanza tu miguu huuma kishenzi
 
Hahaha kuna rafiki yangu kila siku jioni gym ananiambia nitakulipia nikamwambia nipe hiyo hela nikiwa tayari nitaenda amekataa ananiambia we nikupe hela huwezi kwenda yaan angenipa angeisoma no naanzaje mm
[emoji23] [emoji23] [emoji23] we unaweza mazoezi ya kukata viuno maana yale hufundishwi unajikuta tu unajua
 
Back
Top Bottom