Kila nikichemsha njegere haziivi

Kila nikichemsha njegere haziivi

CLONEY

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
104
Reaction score
29
Mwenzenu kila nikipika njegere haziivi je nakosea wapi au nazo zinatofautiana na nyingine huwa haziivi?
 
njegere zipi kavu au mbichi kama ni mbichi mbona huwa azisumbui..
 
kuna aina fulani lazima upike kama maharage, simaanishi yale ya mbeya.
 
Zipikie kwenye Presha Cooker hazitaleta ubishi zitaiva tu tena kwa dakika chache
 
user-offline.png
ndetichia, Duduwasha, bidada na MadameX thanks
 
Njegere zingine ganda lake huwa gumu japo zikiiva unakula kama kaugumu flani. Kumbuka usizifunike ili zisichubuke maganda.
 
okay asante na je unaweza kuifahamu aina hii kwa kuiangalia tu
 
mwenzenu kila nikipika njegere haziivi je nakosea wapi au nazo zinatofautiana na nyingine huwa haziivi?
Mkuu njegere gani hizo unazoziongelea?ni hizihizi (za kawaida) nazozifahamu mimi?
 
okay asante na je unaweza kuifahamu aina hii kwa kuiangalia tu

kuna njegere haziivi wanasema za west kilimanjaro kuziangalia kwa macho ni kubwa na rangi yake zimezidi kijani sijawahi fanya utafiti
 
Ni hizi hizi za kawaida mkuu....,,. mhh halafu avatar yako inatisha

Mkuu niliugua ugonjwa wa ndui ilibaki kidogo nipoteze maisha,ndiyo maana yamebaki madoa madoa usoni!Huu ugonwa uliua watu wengi sasa hapa kwetu Tanzania.
 
zipo njegere zisizoive na hizi mara nyingi sana zinalengwa kupikwa zikiwa kavu kama maharage na sio mbichi. siri moja ukitaka kujua njegere zinazoiva angalia punje zake, punje kubwa na zenye rangi ya kijani ilioiva sana, na ambazo ukizimenya hukuti zina wadudu wale funza wanaokula njegere ujue basi hizi haziivi. ukizitafuna mbichi utaona hazina sukari mdomoni so kama zimemenywa toka sokoni jaribu kuuma moja ama kuangalia aina ya punje.

kwa ambazo zinaiva hizi zina punje ndogo na zimepauka fulan hivi pia kama zina maganda utakuta nyingi zimeliwa na funza kwani zinanoga sukari, njegere hizi unapopika usifunike wala kupika na maji mengi sana zitamenyeka.

unapotaka kupika hizo zinazoiva kwa kutolainika basi zichemshe kwa maji kidogo, bila chumvi, yakikaukia ongeza maji tena, pia zifunike ziive kwa mvuke na usichemshe kwa moto mkali sana zitababuka badala ya kuiva.
 
Back
Top Bottom