zipo njegere zisizoive na hizi mara nyingi sana zinalengwa kupikwa zikiwa kavu kama maharage na sio mbichi. siri moja ukitaka kujua njegere zinazoiva angalia punje zake, punje kubwa na zenye rangi ya kijani ilioiva sana, na ambazo ukizimenya hukuti zina wadudu wale funza wanaokula njegere ujue basi hizi haziivi. ukizitafuna mbichi utaona hazina sukari mdomoni so kama zimemenywa toka sokoni jaribu kuuma moja ama kuangalia aina ya punje.
kwa ambazo zinaiva hizi zina punje ndogo na zimepauka fulan hivi pia kama zina maganda utakuta nyingi zimeliwa na funza kwani zinanoga sukari, njegere hizi unapopika usifunike wala kupika na maji mengi sana zitamenyeka.
unapotaka kupika hizo zinazoiva kwa kutolainika basi zichemshe kwa maji kidogo, bila chumvi, yakikaukia ongeza maji tena, pia zifunike ziive kwa mvuke na usichemshe kwa moto mkali sana zitababuka badala ya kuiva.