Alfred
JF-Expert Member
- Apr 13, 2008
- 2,093
- 2,843
Tumsifu yesu Kristu!
Ee bwana mimi nikienda kanisani huwa najikuta natamani sana kuwa padre, naona kama mapadre ni ma role model wangu, Najikuta nafanya imagination nyingi za kipadre!
Sitaki niwaze ila kila nikiingia kanisani lazima iwe hivyo, kuna roho ya kumuacha hata shemeji yenu inakuja kabisa..
Napagawa kabisa wakati wa mageuzo pale Padre Akisema, Akawapa mkate akisema twaeni mle nyote huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu, kisha akawapa kikombe akisema twaeni mnywe nyote hiki ndicho kikombe cha damu yangu, damu ya agano jipya na la milele itakayomwagika kwa ajili yenu na kwa ajili ya wengi..Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi... Halafu anaponyanyua na Kusema Kwa njia yake pamoja naye ndani yake wewe Mungu Mwenyezi katika Umoja wa Roho mtakatifu unapata heshima na utukufu wote milele hata milele!
Nifanyeje nisipate hizi hisia za Upadre? ila huwa nisipoenda kanisani nakuwa fresh siwazi mambo ya upadre!
Muwe na Jumapili Njema ya Dominika ya 21 ya Mwaka B wa Kanisa!