Kila Nikienda Kanisani lazima nikutane na hili tatizo!

Kila Nikienda Kanisani lazima nikutane na hili tatizo!

Alfred

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2008
Posts
2,093
Reaction score
2,843
Tumsifu yesu Kristu!
Ee bwana mimi nikienda kanisani huwa najikuta natamani sana kuwa padre, naona kama mapadre ni ma role model wangu, Najikuta nafanya imagination nyingi za kipadre!
Sitaki niwaze ila kila nikiingia kanisani lazima iwe hivyo, kuna roho ya kumuacha hata shemeji yenu inakuja kabisa..
Napagawa kabisa wakati wa mageuzo pale Padre Akisema, Akawapa mkate akisema twaeni mle nyote huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwa ajili yenu, kisha akawapa kikombe akisema twaeni mnywe nyote hiki ndicho kikombe cha damu yangu, damu ya agano jipya na la milele itakayomwagika kwa ajili yenu na kwa ajili ya wengi..Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi... Halafu anaponyanyua na Kusema Kwa njia yake pamoja naye ndani yake wewe Mungu Mwenyezi katika Umoja wa Roho mtakatifu unapata heshima na utukufu wote milele hata milele!

Nifanyeje nisipate hizi hisia za Upadre? ila huwa nisipoenda kanisani nakuwa fresh siwazi mambo ya upadre!

Muwe na Jumapili Njema ya Dominika ya 21 ya Mwaka B wa Kanisa!

Alfred
 
Labda ilikua ndicho kitu ulipaswa kufanya badala ya kuoa. By the way hakuna namna ya kuwa padre tena baada ya kuoa. Kupata hizo feelings ni kitu cha kawaida tu. Nenda kanisani endelea kuwa muumini mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
okay basi ni kawaida, ngoja ngoja umri usogee kidogo utapata muafaka wa nini unataka kufanya na wapi unataka kuwa.
Sawa sawa asante Mkuu japo najua ni ngumu maana niko ndani ya carrier saivi
 
Unafanya kazi gani kwa sasa. Niliwahi kushuhudia askari Polisi aliyefanya kazi kwa miaka kumi ikiwa hajaoa na alijikuta anabadili carrier na kuwa padri nothing is impossible

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waulize walioingia huo wito na kuacha watakuelewesha . Usioe au usiolewe ili ufanye kazi ya Mungu !!! Kwani Muumba alikuleta duniani ili ule na kunywa tu !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom