Kila nikiifikiria hii kodi nashindwa kuwaelewa TRA, naona kama naibiwa

Kila nikiifikiria hii kodi nashindwa kuwaelewa TRA, naona kama naibiwa

Nimefungua biashara mwezi wa tisa nikaona ni bora niende TRA ili nifanye biashara kwa kufuata sheria za nchi na nilipe kodi.

Kutokana na biashara yangu nikakadiriwa kodi laki moja na hamsini kwa mwaka; sikuwa na shida na hilo.

Lakini kitu kilichonishangaza baada ya kuprintiwa makaratasi yangu ya makadirio nikaambiwa hiyo laki na hamsini inatakiwa niilipe kabla ya tarehe 31 December

Nikamwambie yule dada biashara nimeanza mwezi huu wa tisa na hizi kodi naona hapa mmezigawanya katika robo 4 mimi inanihusu hi robo ya mwisho sasa kwa nini nilipie na hizo robo 3 kipindi ambacho biashara haikuwepo?

Yule dada akaniambia system ndio imesetiwa hivyo haijalishi biashara umeanza lini unatakiwa ulipe kodi yote ya mwaka mzima

Naomba TRA mnijibu maswali mzima?

1) Nani aliyeiseti hiyo system ya kuwaibia walipa kodi ni kwamba elimu yake ndogo au alifanya kusudi ili kutukomoa tunaotaka kulipa kodi kwa hiyari?

2) Kwa elimu yangu ndogo niliyo nayo kodi inalipwa baada ya kufanya biashara na kupata income sasa iweje mnadai kodi katika kipindi ambacho biashara haikuwepo?

3) mmenikadiria income yangu ni laki tano kwa mwaka ambayo kodi yake ndiyo hiyo laki na hamsini sasa iweje income nitakayo ipata kwa miezi 4 muichaji kodi ya mwaka mzima?

4) Haya mahesabu ya kodi mnayo yafanya ndivyo mlivyo fundishwa huko chuoni kwenu pale kijitonyama au mnatoa kichwani kwenu ili kuwa vunja moyo walipa kodi?View attachment 1278195
UKifuata haki ya kulipa kodi hapa Tanzania utaua biashara.

Kodi za Tanzania zinawanyonya sana wafanyabiashara
 
Hilo ni deni tayari linasoma katika tin namba yangu na natakiwa nililipe kabla ya tarehe 31 December
Nisipo lipa ikifika 2020 nitapigwa penati kwa kweli najuta kwa nini nilienda TRA
Tatizo hatuna elimu ya kodi za serikali maana ungekuwa unajua ungekausha mpaka mwakani
Hapo bado kwenye Leseni nako unatakiwa ukalipe kabla mwaka aujaisha+ service levy+ makorokoro mengine kutegemea na Biashara yako
 
Hutakiwi kukadiriwa kodi na TRA; sheria inakuhitaji wewe mwenyewe ndie upeleke makadirio yako. Ndio maana kukawekwa na penalty (adhabu) endapo itabainika kuwa makadirio yako yalikuwa ni madogo kuliko mapato makubwa (inapotokea tofauti kati ya mapato halisi na makisio ni tofauti angalau kwa 20% au zaidi).
Siku nyingine tafuta mhasibu akusaidie.
Kupeleka hesabu ni mpaka uwe na kampuni
Kwa sole propr unakadiriwa na wao
 
Kuna haja gani ya kupeleka makadirio, si wangesubiri mapato halisi ili wachukue kodi kutoka hapo? Maana kama mtu anapewa adhabu kwa kukadiria chini ya uhalisia, atajua aje mapato halisi ikiwa hajafanya biashara yenyewe?
 
Mkuu unajua kweli unachokiongea ?, Certified accountant akikufanyia mahesabu mara nyingi bei yake ni kwenye laki tatu sasa mtu kodi yake imekadiriwa na TRA kama ni laki na nusu alipe laki tatu ili akadiliwe laki na nusu ?

TRA wanakadilia accordingly na band za mauzo tofauti tofauti kwa mwaka yana gharama zake elekezi, cha kufanya ili usipunjwe inabidi uwe unatunza mahesabu na risiti ili wakuchaji accordingly bila hayo mahesabu wanakadiria accordingly na watakavyoona kulingana na duka, biashara na sehemu husika (kumbu ni mauzo na sio faida inayopigiwa kodi).., na Kodi inachajiwa kwa mwaka ingawa unaruhusiwa kulipa installments nne (kwahio ukianza kazi hata desemba 1 utachajiwa installment zote kuanzia mwanzo wa mwaka
Je utaratibu huu unaleta mantiki? Ndicho anacholalamikia mleta mada. Au ni lazima kila biashara ianze shughuli zake mwanzo wa mwaka?
 
Wananidai 8.4mil baada ya kutolipa kodi ya kadrio la 1.5mil kwa mwaka kwa miaka 4 na penalty
Uhalisia ukoje? Je biashara ina mauzo kama waliyokadiria?
 
Hilo ni deni tayari linasoma katika tin namba yangu na natakiwa nililipe kabla ya tarehe 31 December
Nisipo lipa ikifika 2020 nitapigwa penati kwa kweli najuta kwa nini nilienda TRA
Mkuu ulijipeleka kikaangoni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asante kwa ubishi wenu nimeongeza kitu pale nilipokuwa naishia ingawa KeyserSoze umetoa jedwali la PAYE kama total income tax. Kitu ambacho sioni kama ni sahihi
 
Na barua ya MJUMBE nayo yatakua ilipiwe [emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo hatuna elimu ya kodi za serikali maana ungekuwa unajua ungekausha mpaka mwakani
Hapo bado kwenye Leseni nako unatakiwa ukalipe kabla mwaka aujaisha+ service levy+ makorokoro mengine kutegemea na Biashara yako
 
wewe ndiyo uliyekosea timing ya kujipeleka huko TRA.ungesubiri hadi January ndiyo uende, but saiv umeenda system yao haitambui kama ni mwisho wa mwaka au lah.huyo dada kakuelekeza sahihi kabisa.na ukisema usiilipe hiyo kodi uliyokadiriwa ikifika mwakani itakuwa deni,watakusumbua mpaka ukome.
 
Alitaka muongee pembeni. Dada wa TRA washenzi sana. Hapo ungemhonga kumi tu angekuambia njoo ulipe machi 2020
 
Kama bado hujapata suluhisho ya hili tatizo, jibu ni hili.
Andika barua TRA kuwa huwezi lipa kodi quarter 1, 2 na 3 kwa kuwa biashara ilikuwa haijaanza. Weka na TIN yako. Toa copy na hakikisha umeweka sahihi yako. Ipeleke hiyo barua hapo.

Kinachotokea, hutolipa kodi ya hizo 3, utalipa quarter ya 4 tu. Wataichukua hizo barua na kupiga mhuri, moja watabaki nayo, nyingine utaondoka nayo.

Mchezo umeisha.
Hasante kwa ushauri nitaandika hiyo barua na kuwalipa 37500 ndio haki yao
 
Kuna haja gani ya kupeleka makadirio, si wangesubiri mapato halisi ili wachukue kodi kutoka hapo? Maana kama mtu anapewa adhabu kwa kukadiria chini ya uhalisia, atajua aje mapato halisi ikiwa hajafanya biashara yenyewe?

Ni njia ya kukusanya mapato, na ndio maana mlipakodi anapewa nafasi ajikadirie kwa kuwa ni yeye anaeifahamu biashara yake. Kukiwa na mabadiliko unajaza tena revised estimates ili kukwepa adhabu.
 
Kupeleka hesabu ni mpaka uwe na kampuni
Kwa sole propr unakadiriwa na wao

Nope. Hata sole proprietor anapaswa kutengeneza hesabu (kwa hiari akitaka au kwa lazima kama mauzo yake yanazidi 100m kwa mwaka).
 
wewe ndiyo uliyekosea timing ya kujipeleka huko TRA.ungesubiri hadi January ndiyo uende, but saiv umeenda system yao haitambui kama ni mwisho wa mwaka au lah.huyo dada kakuelekeza sahihi kabisa.na ukisema usiilipe hiyo kodi uliyokadiriwa ikifika mwakani itakuwa deni,watakusumbua mpaka ukome.
Mimi sina kosa wao na system yao ndio shida
Hi biashara nimemfungulia wife sasa nikaona sio vizuri anze kukimbizana na tra au jiji ni bora nifuate taratibu zote za kisheria ili akikaa katika biashara akae kwa amani
 
Nope. Hata sole proprietor anapaswa kutengeneza hesabu (kwa hiari akitaka au kwa lazima kama mauzo yake yanazidi 100m kwa mwaka).

Uko sahihi but hata kama hajafikisha anaweza fanya application kwa Commissioner General. Tatizo lipo kwa hawa wasopeleka yaani presumptive taxpayers wao kodi inakadiriwa kutokana na mauzo na sio profit.
 
Back
Top Bottom