Kila nikiifikiria hii kodi nashindwa kuwaelewa TRA, naona kama naibiwa

UKifuata haki ya kulipa kodi hapa Tanzania utaua biashara.

Kodi za Tanzania zinawanyonya sana wafanyabiashara
 
Hilo ni deni tayari linasoma katika tin namba yangu na natakiwa nililipe kabla ya tarehe 31 December
Nisipo lipa ikifika 2020 nitapigwa penati kwa kweli najuta kwa nini nilienda TRA
Tatizo hatuna elimu ya kodi za serikali maana ungekuwa unajua ungekausha mpaka mwakani
Hapo bado kwenye Leseni nako unatakiwa ukalipe kabla mwaka aujaisha+ service levy+ makorokoro mengine kutegemea na Biashara yako
 
Kupeleka hesabu ni mpaka uwe na kampuni
Kwa sole propr unakadiriwa na wao
 
Kuna haja gani ya kupeleka makadirio, si wangesubiri mapato halisi ili wachukue kodi kutoka hapo? Maana kama mtu anapewa adhabu kwa kukadiria chini ya uhalisia, atajua aje mapato halisi ikiwa hajafanya biashara yenyewe?
 
Je utaratibu huu unaleta mantiki? Ndicho anacholalamikia mleta mada. Au ni lazima kila biashara ianze shughuli zake mwanzo wa mwaka?
 
Wananidai 8.4mil baada ya kutolipa kodi ya kadrio la 1.5mil kwa mwaka kwa miaka 4 na penalty
Uhalisia ukoje? Je biashara ina mauzo kama waliyokadiria?
 
Hilo ni deni tayari linasoma katika tin namba yangu na natakiwa nililipe kabla ya tarehe 31 December
Nisipo lipa ikifika 2020 nitapigwa penati kwa kweli najuta kwa nini nilienda TRA
Mkuu ulijipeleka kikaangoni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asante kwa ubishi wenu nimeongeza kitu pale nilipokuwa naishia ingawa KeyserSoze umetoa jedwali la PAYE kama total income tax. Kitu ambacho sioni kama ni sahihi
 
Na barua ya MJUMBE nayo yatakua ilipiwe [emoji23][emoji23][emoji23]
Tatizo hatuna elimu ya kodi za serikali maana ungekuwa unajua ungekausha mpaka mwakani
Hapo bado kwenye Leseni nako unatakiwa ukalipe kabla mwaka aujaisha+ service levy+ makorokoro mengine kutegemea na Biashara yako
 
wewe ndiyo uliyekosea timing ya kujipeleka huko TRA.ungesubiri hadi January ndiyo uende, but saiv umeenda system yao haitambui kama ni mwisho wa mwaka au lah.huyo dada kakuelekeza sahihi kabisa.na ukisema usiilipe hiyo kodi uliyokadiriwa ikifika mwakani itakuwa deni,watakusumbua mpaka ukome.
 
Alitaka muongee pembeni. Dada wa TRA washenzi sana. Hapo ungemhonga kumi tu angekuambia njoo ulipe machi 2020
 
Hasante kwa ushauri nitaandika hiyo barua na kuwalipa 37500 ndio haki yao
 
Kuna haja gani ya kupeleka makadirio, si wangesubiri mapato halisi ili wachukue kodi kutoka hapo? Maana kama mtu anapewa adhabu kwa kukadiria chini ya uhalisia, atajua aje mapato halisi ikiwa hajafanya biashara yenyewe?

Ni njia ya kukusanya mapato, na ndio maana mlipakodi anapewa nafasi ajikadirie kwa kuwa ni yeye anaeifahamu biashara yake. Kukiwa na mabadiliko unajaza tena revised estimates ili kukwepa adhabu.
 
Kupeleka hesabu ni mpaka uwe na kampuni
Kwa sole propr unakadiriwa na wao

Nope. Hata sole proprietor anapaswa kutengeneza hesabu (kwa hiari akitaka au kwa lazima kama mauzo yake yanazidi 100m kwa mwaka).
 
Mimi sina kosa wao na system yao ndio shida
Hi biashara nimemfungulia wife sasa nikaona sio vizuri anze kukimbizana na tra au jiji ni bora nifuate taratibu zote za kisheria ili akikaa katika biashara akae kwa amani
 
Nope. Hata sole proprietor anapaswa kutengeneza hesabu (kwa hiari akitaka au kwa lazima kama mauzo yake yanazidi 100m kwa mwaka).

Uko sahihi but hata kama hajafikisha anaweza fanya application kwa Commissioner General. Tatizo lipo kwa hawa wasopeleka yaani presumptive taxpayers wao kodi inakadiriwa kutokana na mauzo na sio profit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…