kunguni wa ulaya
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 4,131
- 6,111
Mimi nimeanza biashara mwezi wa 4 mwaka huu,Kwakweli maofisa wa TRA sijui ni rushwa au sijui wamekaaje? Wakija kukukadilia kodi hukubambikia makadirio yasiyokuwa ya uhalisia hata kodi ya pango nayo wanaipigia kodi na ukilalamika wanasema eti system imesettiwa hivyo! Hayo nimekutana nayo saana hila huwa nakomaaa na kutaka kuongea na Meneja mpaka wanaachia! Komaa nao vyinginevyo itakula kwako!
1. Nilitakiwa nilipe na kodi ya quarter ya kwanza kama mleta mada anavyolalamika.
2. Tax officer kanikadiria kodi ila bosi wake kasema hii haimtoshi muongezee. Nikalalamika akasema utake utalipa usitake utalipa.
Chakushangazaa yule alienihoji kujusu hako kabiashara kangu kapya kanielewa ila yule bosi wake kagoma kunielewa.
3. Nikalipa instalmnt 1 kisha nikaandika barua kuomba nifanyiwe assesment upya kutokana na hali ya biashara kuwa ngumu. Meneja akagoma akasema lipia installment zilizobaki kisha ndio tunaweza kukubadilishia.
4. Nimeamua wiki hii napeleka barua ya kusitisha TIN yangu kuwa nafunga biashara. Tuone hata kile kidogo ambacho nilikua na uwezo nacho wa kulipia hawatakipata.
Nadhani watu wa TRA na serikali wanapita humu wataona malalamiko yetu.
Kama jiwe ndii kawalazikisha wafanye kazi kwa staili hii basi analazimisha watu wote tukalime na tuachane na biashara na kujiajiri.