Kila nikijaribu kumsamehe/kuwasamehe nashindwa

Nimesoma yote mstari baada ya mstari maana haichoshi kusoma.

Pole Mkuu kwa yote uliyopitia Mungu akutunze na wanao.
 
Bro unajua uzuri wa JF unatoa ushauri ambao haupo biased. Mimi sikufahamu ila nimejaribu kusema hayo ili kama kuna next time ( sikuombei ) ubadilike au vilevile umwangalie yule mwanamke kwa jicho la pili ( sio kurudiana.

Ishu za kusaidia kwao mbona ni kawaida, wewe waliokusaidia leo hii wakiwa wanakumbushia misaada yao utajisikiaje?

Kuna watu misaada yao huwa inawafanya wajisikie vizuri, natumaini wewe sio mmoja wao.

Nilikuwa na rafiki yangu mmoja alikuwa anapenda kujisifia kweli. Kila kitu chake ni kizuri, ataongea gari langu hivi, kazi yangu hivi, kwetu hivi, mchepuko wangu hivi e.t.c.
But trust me hio tabia inaboa, na watu wa hivyo ni ngumu sana kuishi nao. Utakuta mume anacomment kila kitu hadi chumvi [emoji3][emoji3]

Mzee sisemi kwamba na wewe upo hivyo, ila nimejaribu kuwa neutral na kuiapproach story yako kwenye angle hiyo.

Take home message, fanya self-reflection, uone kama kuna ya kuboresha, na trust me siku zote huwa yapo.
 
Vitu vyenyewe vitu gani bro ? Vitanda na TV ya inch 32?
Kuna watu wanaacha magari na nyumba na hawalalamiki.
Kama una hela kweli hivyo vitu si unareplace tu.
Kwanza mlitaka asepe bila kitu kabisa ?
 
Vitu vyenyewe vitu gani bro ? Vitanda na TV ya inch 32?
Kuna watu wanaacha magari na nyumba na hawalalamiki.
Kama una hela kweli hivyo vitu si unareplace tu.
Kwanza mlitaka asepe bila kitu kabisa ?
Ndio uone maamuzi ya kijinga yalivyomcost huyo mdada, kwani aivyouza vitu akaondoka si aliona hatarudi tena!? Sasa nn kinachomrudisha kuomba msamaha!???

Mkuu jamaa hapa kama nimeelewa halalamikii vitu bali ameeleza mkasa mzima hadi alivyochukuwa wanae, ndio maana hakwenda hata polisi kushtaki au kudai mali
 
Hahaha kweli tunatofautiana aisee ningekuwa keko mida hii. Sijui kama ningekuwa nmeshahukumiwa au la ila najua ningekuwa wapi muda huu.
 
Funguka kidogo ili ndugu zako tupate maarifa zaidi juu ya hivi viumbe Bosi
 
Aiseee sijui wewe ni dada au kaka ila umenisikitisha sana! Binafsi nimeumia mnoo hivi najiuliza huyo mwanamke akili yake ipo sawa kweli? Hata kama mumeo alikucheat na ukagundua kwahiyo ndo ufanye malipizi kisa mume kakucheat na wewe ufanye the same thing? Mbaya zaidi upo kwenye serious relationship na watoto wawili umezaa? Alishindwa kuwafikiria watoto wake?

Mjinga hapo ni mwanamke no matter what hauwezi kushindwa kuwaangalia watoto wako tena wa kuwazaa mwenyewe kwa uchungu kisa mwanaume kacheat au umkomee mwanaume huo ni uzwazwa wa hali ya juu! Cha msingi mwanaume awe anajali familia yake! Hayo mengine ni ujinga wa kujitakia.

Then don’t call him mpumbavu while you are the one ambae ndo mpumbavu hata kufikiria umeshindwa! Shame on you
 
Pole sana, mkuu kiukweli una moyo!

Kikubwa msamehe tu lakini usijiroge kurudiana nae.
 
2014-2015 Nililia lia saaana humu japo nilikuwa na ID nyingine, kuliaccept hilo jambo nilichukua mwaka mmoja, baada ya mwaka nikubali she has gone!! Nikabadili plans zangu za maisha! Ila niliumia saaana
Ilikuwaje kaka? coz hakuna bingwa wa mapenzi na ambaye hakuwahi kupitia changamoto kama hizo, so naomba kujua chanzo cha mkasa
 
Kama mtu hajawahi changamoto kama hizi anaweza kudhani ni hadithi za kutunga.
Tena afadhali wew maumivu yako sio makubwa kama yangu, story kwa ufupi mke wangu kwa kushirikiana na familia yake waliuza kila kitu nyumba hadi gari na mtoto niliambiwa sio wangu na kweli mtoto alikuwa sio wangu kuja kufuatilia kumbe nilioa mwanamke akiwa na ujauzito wa mwezi mmoja.
Baada ya miezi 2 kurudi Tz kupeleleza nikagundua mwanamke yupo kwa bwana ake aliyemzalisha uyo mtoto.
Nikafungua kesi ya wizi mahakamani, mpka muda muda huu ndugu wa mwanamke, mwanamke mwenyewe pamoja na bwana ake wapo segerea mwaka 1.5 huu na warudishe mali zangu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…