Naomba nieleweke simaanishi kuwa wanuka kinywa, bali yawezekana mwanadada huyo ana ile hali ya kuhisi kinyaa kwa kuwa wapo watu wa hivyo. Nikupe pole tu hapa maana najua hata BJ itakuwa unatoka kapa.
Japo ikitokea tatizo likawa ni kunuka kinywa jitahidi usafishe kinywa chako vizuri. Jitahidi kila unapokula uswaki vizuri na hakikisha unasugugua vizuri ulimi wako kila sehemu mpaka na juu ya cavity(juu ya kinywa). Kwenye ulimi zingatia sana.
Vya kuzingatia;
Asubuhi: Mswaki ni lazima upige asubuhi ukiamka, baada ya chai waweza pitisha mswaki bila hata ya kuweka dawa ya meno(exception ukila vyakula shombo kama samaki tumia dawa) kuondoa mabaki ya chakula.
Mchana: Mara nyingi watu huwa busy kwenye shughuli za utafutaji kwa hiyo jitahidi uwe na hata bablishi (hasa PK au hata ambazo hazina sukari ndio nzuri zaidi) tumia umalizapo kula, inasaidia kuondoa mabaki ya chakula yaliyonasia mdomoni hasa katika meno.
Usiku: Hakikisha kabla hujalala unaswaki iwe umekula kitu au hujala lazima uswaki.
NB: Hali ikiendelea kuwa mbaya nenda kwa daktari wa meno